QUICK DELIVERY
Swift dispatch
ONLINE PAYMENT
Multiple options
EXPERT SUPPORT
Help when you need it
WIDE VARIETY
Thousands of books
GLOBAL SHIPPING
Worldwide delivery
0794 233 261
Yananiandama na Hadithi Nyingine ni mkusanyiko wa hadithi fupi zinazolenga hadhira ya wanafunzi, wasomaji wa kawaida na wataalamu wowote wale. Huu ni mkusanyiko unaowaleta pamoja waandishi walio na viwango vya juu vya ubunifu na ukwasi wa lugha. Hadithi zilizomo kwa ujumla zinagusa nafasi na nafsi ya msomaji. Bila shaka, msomaji yeyote wa mkusanyiko huu atagundua kuwa waandishi wake ni wenye uwezo mkubwa katika utunzi, fauka ya kuwa wengine wao wanalimbukia fasihi andishi. Naam, ulimbukeni wao umeleta sura ngeni katika ulimwengu wa fasihi andishi.
Jeff Mandila ni mmoja wa waandishi wanaoinukia kwa kasi mno. Ni mwandishi wa riwaya, tamthilia na hadithi fupi kando na utunzi wa mashairi. Alizaliwa karibu na mji wa Kitale mwaka wa 1985. Alijishindia tuzo ya Wahome Mutahi 2012 baada ya riwaya yake ya Sikitiko la Sambaya kuibuka ya kwanza.
Geoffrey Mung’ou ambaye pia ni mwandishi wa riwaya ya Mkakasi ni mhariri katika Shirika la Habari la Standard. Ana shahada katika kitivo cha Elimu (Kiswahili na Historia-Chuo Kikuu cha Kenyatta). Ametoa mchango mkubwa kuhusu Kiswahili katika vyombo vya habari, kwenye makongamano na shuleni. Aidha, amekuwa mwalimu wa somo la Kiswahili katika shule kadhaa za upili nchini Kenya. Mbali na kazi hizi za fasihi, ameibukia na vitabu adhimu kuhusu fani nyinginezo za lugha.
Nimepoteza Tena na Hadithi Nyingine ni mkusanyiko wa hadithi fupi zinazolenga hadhira ya wanafunzi, wasomaji wa kawaida na wataalamu wowote wale. Huu ni mkusanyiko unaowaleta pamoja waandishi walio na viwango vya juu vya ubunifu na ukwasi wa lugha. Hadithi zilizomo kwa ujumla zinagusa nafasi na nafsi ya msomaji. Bila shaka, msomaji yeyote wa mkusanyiko huu atagundua kuwa waandishi wake ni wenye uwezo mkubwa katika utunzi, fauka ya kuwa wengine wao wanalimbukia fasihi andishi. Naam, ulimbukeni wao umeleta sura ngeni katika ulimwengu wa fasihi andishi.
Kikechi Kombo B. ana Shahada ya elimu na sanaa na shahada ya uzamili kutoka Chuo Kikuu cha Kenyatta. Ni mwalimu mwenye tajiriba pana katika lugha na fasihi ya Kiswahili kwa miaka mingi. Hushiriki uchambuzi wa lugha na fasihi katika Idhaa ya Radio Taifa- KBC. Ameandika vitabu vya marudio katika lugha ya Kiswahili na miongozo tolatola mathalan mwongozo wa Chozi la Heri, mwongozo wa Kigogo, mwongozo wa Kidagaa Kimemwozea na mwongozo wa Mstahiki Meya. Amechangia pia katika kitabu cha marudio cha Kioo Cha KCSE, Mwongozo wa Nguu za Jadi na Mapambazuko ya Machweo na hadithi nyingine miongoni mwa vitabu vingine.
Kenna Wasike ni mwandishi wa kazi za fasihi. Ameandika kazi aula za bunilizi. Aidha, amechangia katika uandishi wa hadithi fupi. Hadithi yake maarufu ni ‘Mapenzi ya Kifaurongo’ katika mkusanyiko wa Tumbo Lisiloshiba na Hadithi Nyingine. Vilevile, amechangia katika uandishi wa kitabu cha marudio ya fasihi. Kwa sasa yeye ni mwalimu wa Kiswahili katika Shule ya wavulana ya Chesamisi iliyoko gatuzi la Bungoma nchini Kenya.
Mzee Kambirani na Hadithi Nyingine ni mkusanyiko wa hadithi fupi zinazolenga hadhira ya wanafunzi, wasomaji wa kawaida na wataalamu wowote wale. Huu ni mkusanyiko unaowaleta pamoja waandishi walio na viwango vya juu vya ubunifu na ukwasi wa lugha. Hadithi zilizomo kwa ujumla zinagusa nafasi na nafsi ya msomaji. Bila shaka, msomaji yeyote wa mkusanyiko huu atagundua kuwa waandishi wake ni wenye uwezo mkubwa katika utunzi, fauka ya kuwa wengine wao wanalimbukia fasihi andishi. Naam, ulimbukeni wao umeleta sura ngeni katika ulimwengu wa fasihi andishi.
These stories are colourfully narrated in a charming and fast moving chronicle about noticeable issues that are close to many people’s emotions. The issues include love, school, family, relationships and diseases among many other contemporary concerns.
The stories unveil a great deal of originality with a striking style.
The book is a must read for students and junior readers.
Swift dispatch
Multiple options
Help when you need it
Thousands of books
Worldwide delivery
No account yet?
Create an Account