Showing all 3 results

Sauti ya Dhiki

KShs13,500.00
Diwani hii - inayosheheni mashairi kuhusu utamaduni, mapenzi, nasaha, siasa, mambo ya kinyumbani, n.k. - ilitungwa baina ya 1969 na 1972 ambapo mtunzi alikuwa kifungoni baada ya kupatikana na hatia ya kuwachochea watu ili waipindue Serikali ya Kenya kwa kutumia silaha. Kwa hivyo, unapoisoma diwani hii hutaweza kujizuia kuona athari ambayo kifungo huweza kuwa nayo kwa mfungwa. n nJambo la maana sana kuhusu diwani hii ni kwamba mtunzi ameweza kuzungumzia mambo ya kisasa, kama alivyofanya katika shairi la 'Usiniuwe!', bila kupotoka na kutafuta mifano ya kigeni. Hili ndilo lililompa Shihabuddin Chiraghdin, mmoja wa wataalamu mashuhuri wa lugha ya Kiswahili, kusema katika utangulizi wake kwamba, ingawa mtunzi ameingiliwa na athari za kigeni kwa ajili ya elimu aliyoipata shuleni, 'hakukubali kuzongwazongwa na athari hizo, hivyo mashairi yake hayana maingilio ya miundo ya kigeni hata chembe, na mawazo yake yote yameambatana na Uswahili na Uafrika kwa jumla'. n nKitabu hiki kitawafaa wale wapendao kusoma mashairi ya Kiswahili ya kiwango cha juu, na vilevile wanafunzi wa fasihi ya Kiswahili katika shule za sekondari na vyuo vikuu.

Nyota ya Rehema

KShs11,000.00
Kwa nini Rehema alizaliwa tofauti na wazazi wake . . . ? Kwa nini alichaguliwa yeye kuwa ni ‘fumbo’? n nla maumbile . . . ? Na kwa nini alifika duniani pale mama yake alipokuwa kapigwa na bumbuazi; baba yake yu katika hali iliyoelezewa kuwa huwafanya walioweka ahadi wazivunje, mashujaa wapoteze nguvu zao, matajiri wajione wahitaji, wenye macho wageuke pofu . . . ? Lakini hiyo ndiyo nyota ya Rehema. n nllichomoza pale tete ya uzazi ilipotunga tumboni mwa mamaye. llimwongoza katika kiza cha majaaliwa– njia ya lazima kwa kila mja–akaifuata pasi na hiari. Vioja na vituko, siku nenda siku rudi, mpaka hatimaye amri isiyopingika ikasema, ho! Hapo ndiyo mwisho . . . .

Introduction to East African Poetry

KShs20,000.00
Author: Jonathan Kariara ISBN: “9780195723793”