Hakuna kitabu kimoja cha Kiswahili kinachoshughulikia mbinu na· mikakati ya kufundisha mada mbalimbali za lugha na fasihi. Mbinu za Kisasa za Kufundishia Kiswc/lh,ili ni ki,tabu kinachoshughulikia ufundishaji wa Kiswahili. Kitabu hiki kinabainisha na kufafanua mbinu ta kisasa za kufundishia mada kama: matamshi, sarufi, msamiati, ufahamu, insha na fasihi. Dhana muhimu katika ufundishaji wa lugha na fasihi zinafafanuliwa na kutolewa mifano mwafaka inayotokana na tajriba ndefu ya waandishi wa kitabu hiki katika ufundishaji wa Kiswahili. Kitabu hiki kitawafaa walimu wa shule za msingi, za upili na vyuo.
Oaktari Paul M. Musau ni Mhadhiri Mkuu katika ldara ya Kiswahili Chuo Kikuu cha Kenyatta. Amewahi kuwa Mwenyekiti wa ldara ya Kiswahili katika chuo hicho. Ana shahada za B.Ed. (Nairobi), M.A (Nairobi), na Ph.D (Bay-reuth, Ujerumani). Amewahi kufundisha katika Shule ya Sekondari ya St Charles Lwanga, Kitui na Chuo cha Walimu cha Thogoto.
Leonard Chacha ni mhadhiri katika ldara ya Kiswahili na Lugha za Kiafrika, Chuo Kikuu cha Kenyatta. Amekuwa mwalimu wa Kiswahili katika shule za upili kwa muda mrefu. Ana shahada za Dip. Ed. _(Siriba), B.Ed. (Moi) na M.A. (Kenyatta).