Madhumuni ya kuandika kitabu hiki ni kumrahisishia mwalimu na mwanafunzi kazi na kumpa mwelekeo unaofaa. Kitabu hiki kimeangazia masuala ibuka katika utahini wa karatasi ya tatu ya Kiswahili katika mtihani wa KCSE. Kitabu hiki kimejumuisha vipengele saba vya uhakiki wa fasihi andishi kama vile; Ploti ya tamthilia, dhamira ya mwandishi, mandhari na umuhimu wake, ufaafu wa anwani, maudhui, wahusika na uhusika na mbinu za lugha.
Maswali ya udurusu pia yamejumuisha katika kila mwisho wa onyesho ambayo yatamsaidia mwanafunzi kujinoa na kujipima ratili uelewa wake wa ploti. Maswali ya kiwango cha kitaifa pia yamejumuisha pamoja na majibu yake.
Masuala ibuka kama vile umuhimu wa wahusika, mbinu za kimtindo, aina za takriri, aina za taswira, na vipengele vingine.