Showing all 20 results

Focus on English For Sec Form 1SB

KShs13,000.00
Author:  ISBN: “9789976466300”

Mwangaza wa Kiswahili Kidato 1SB

KShs11,000.00
Author:  ISBN: “9789976466256”

Focus on Civics for Sec Form 1SB

KShs9,500.00
Author:  ISBN: “9789976466218”

Focus on History for Form 1SB

KShs9,500.00
Author:  ISBN: “9789976466171”

Focus on Biology for Sec Form 1SB

KShs13,000.00
Author:  ISBN: “9789976466133”

Focus on Chemistry for Sec Form 1 LB

KShs12,500.00
'The Focus on Chemistry' series takes learners on an exciting journey through the captivating world of Chemistry. The series comprehensively covers the Chemistry syllabus and provides practical experiences that support the acquisition of skills in the new Competency-Based Curriculum.

Focus on Geography for Sec Form 1SB

KShs10,000.00
Author:  ISBN: “9789976466010”

Focus on Mathematics for Sec Form 1SB

KShs13,000.00
Author:  ISBN: “9789976465976”

Musa na Bahati Nasibu

KShs7,500.00
Musa na King Kong wanakumbwa na uhitaji mkubwa wa pesa. Ili kukidhi haja hii, wanaibuka na wazo la kuandaa mchezo wa bahati nasibu. n nMusa analazimika kutafuta zawadi ya kushindaniwa katika shule yao, Mukibi's Educational Institute for the Sons of African Gentlemen. n nIngawa wanafanikiwa kupata zawadi - gari kutoka kwa Nick Molo - mchezo wao unakumbwa na mashaka. n nKwanza, mwalimu mkuu, Mzee Mukibi, anawapokonya tiketi za mchezo. Kisha, inabainika kuwa gari lenyewe ni la kuibwa. n nPesa wanazozipata nazo zinaishia mikononi mwa hasimu wao ...

Musa Mpigakambi

KShs7,500.00
Musa na King Kong wanabaki bila mahali pa kulala baada ya ‘maonesho’ yao ya fataki kuteketeza kimakosa mabweni katika shule yao _ Mukibi's Educational Institute for the Sons of African Gentlemen. Walioathiriwa na mkasa huo wanalazimika kupiga kambi kwenye mahema ukingoni mwa mto. n nKatika harakati za kuchimba shimo la kutia mhimili wa hema, King Kong anachimbua mfuko wenye vito vya thamani. Pamoja na wenzake, wanashindwa kujiwekea siri ya ugunduzi huo mkuu, na muda si mrefu, wanajipata katika matatizo makubwa.

Musa Kwenye Harakati

KShs7,500.00
Wanafunzi katika Mukibi's Educational Institute for the Sons of African Gentlemen wanaenda nyumbani kwa likizo fupi. Hata hivyo. Musa na King Kong wana mpango tofauti. Wanaamua kuitumia fursa hiyo kujifurahisha mjini Tororo. n nWakiwa mjini Tororo, wanakutana na Finito anayewashawishi washiriki katika 'hafla' yake ya uponyaji (kwa malipo) na wanakubali. Musa anapanda jukwaani. Anapogeuka kuutazama umati uliojaa fujo, anakabiliana ana kwa ana na naibu wa mwalimu mkuu, Bw Karanja. Baada ya kufaulu kutoroka, na hata kuwakwepa polisi, wanaapa kufanya juu chini ili kuvuka mpaka. Je, hatima yao itakuwaje?

Musa na Rafiki wa Barua

KShs7,500.00
Ari ya kuwasiliana na marafiki wa barua inashabikiwa sana katika Mukibi's Educational Institute for the Sons of African Gentlemen. Si ajabu kwamba Musa na King Kong wamo katika wimbi hilo la msisimko. n nKando na hayo, Kasali — mvulana mgeni — anatengeneza mvinyo kwa mashine aliyoificha kwenye bweni. Kila anayeuonja anakiri kwamba ni mvinyo mzuri sana, na hata kuhusudu hall ya baadaye ya Kasali katika biashara ya mvinyo. Hata hivyo, majaribio anayoifanyia fomyula ya mvinyo huo inabadilisha pakubwa historia ya Taasisi ya Mukibi.

Musa na Shamba la Shule

KShs7,500.00
Wazo la kuanzisha shamba la shule linawafanya wanafunzi wa Mukibi's Educational Institute for the Sons of African Gentlemen kuandaa mgomo baridi. Kwa madai yao wenyewe, wako shuleni 'kusomea mitihani' wala si kuwa mashokoa wa mwalimu mkuu, Mzee Mukibi. Hata hivyo, hakuna aliye tayari kumkabili mwalimu mkuu kwa kuhofia kuonekana muasi. Masaibu ya Musa na marafiki zake yanazidi kufuatia 'kutoweka' kwa nguruwe dume, na kuku sita kuibwa. Mwalimu mkuu naye ameapa kufanya juu chini kuwanasa wezi.

Moses in Trouble

KShs460.00

It's nothing new for Moses to be in trouble. This time it all begins when he and his friends at Mukibi's Educational Institute for the Sons of African Gentlemen stage a lighthearted protest about the school food.

Moses in a Muddle

KShs460.00
"A girl student in a place like this would be scandalous!" exclaims Mr Karanja, deputy headmaster of Mukibi's Educational Institute for the Sons of African Gentlemen. Mr Mukibi, however, thinks it is a splendid idea and so do the boys when they hear the sensational news. n nMoses and King Kong, who are the first to meet Juli Sekabanja, are not so sure. But Juli has decided that the two friends are just the allies she needs to help her catch a gang of spies she claims to have discovered. Thinking of their share of the reward, they agree. n nBy the end of this hilarious adventure, even Mr Mukibi has changed his mind about the merits of co-education!

Musa Kwenye Sokomoko

KShs7,500.00
"Kumleta mwanafunzi wa kike mahali kama hapa huenda kukawa balaa kubwa!" anasema Bw. Karanja, naibu wa mwalimu mkuu katika Mukibi's Educational Institute for the Sons of African Gentlemen. Bw. Mukibi, hata hivyo anaiona hiyo kuwa hatua nzuri sawa na wavulana wa shule hiyo pindi wanapopata habari hizo za kusisimua. n nJuli Sekabanja anaamua kwamba Musa na King Kong ndio wahusika hasa anaowahitaji ili kumsaidia kunasa genge la majasusi. n n"Musa kwenye Sokomoko" ni hadithi ya tano katika msururu wa "Visa na Vituko vya Musa", vilivyoandikwa na Barbara Kimenye.

Musa na Pepo

KShs7,500.00
Musa, King Kong na wanafunzi wengine wa Bweni nambari 3 hawaamini kwamba kuna pepo. Lakini gimba hili la kutisha linalonyapanyapa kwenye uga wa shule yao ni kitu gani? Madoadoa ya ajabu ya 'damu' yametoka wapi? Na ni nani anayetoa kicheko cha kutisha nje ya mlango wa nyumba ya Bi. Namukasa? Naibu wa mwalimu mkuu, Bw. Karanja, anaamini kuwa ni wanafunzi wa Bweni nambari 3 wanaofanya mzaha. Kwa hivyo Musa na wenzake wanaamua kufanya juu chini kumnasa pepo huyu la sivyo atawafanya watimuliwe shule. "Musa na Pepo" ni kitabu cha sita katika msururu wa "Visa na Vituko vya Musa", vilivyoandikwa na Barbara Kimenye.

Musa na Mildred

KShs7,500.00
Musa anatarajia mambo yamwendee vyema muhula huu, kinyume na masaibu yaliyotawala muhula wa kwanza katika Mukibi's Educational Institute for the Sons of African Gentlemen. Ana matumaini ya kumwonesha rafiki yake, King Kong, kipenzi chake, Mildred. Hata hivyo, mambo yanaanza vibaya na kutumbukia nyongo. Kwanza, kuna mvutana mgeni, Magara, ambaye ni dhatirnu. Kisha, King Kong anabwagwa kwenye kinyang'anyiro cha kiranja wa bweni. Halafu, Mildred anatoweka. n n"Musa na Mildred" ni kitabu cha pill katika msururu wa "Visa no Vituko vya Musa", vilivyoandikwa na Barbara Kimenye.

Musa Mashakani

KShs550.00
"Visa na Vituko vya Musa" ni tafsiri ya Moses Series vilivyoandikwa na Barbara Kimenye, na ambavyo vinaangazia hali ya maisha ya wanafunzi shuleni mwao. Mbali na kuwa vinaburudisha na kuchekesha kwa visa mbalimbali vinavyomkumba Musa, yapo mafunzo mengi anayopata msomaji. Tafsiri hizi zinadumisha mvuto na mnato wa kazi asilia, na zitakupa shauku ya kusoma hadithi yote ili kujua hatima ya kisa chenyewe. Si jambo geni kwa Musa kuwa mashakani. Safari hii, yeye na marafiki zake katika Mukibi's Educational Institute for the Sons of African Gentlemen wanafanya mgomo wa kimzaha kuhusu chakula wanachopewa shuleni. Mwanzoni, wanauona mzaha huo kuwa murua. Hata hivyo, Mwalimu mkuu, Bw. Mukibi, hafurahishwi – yeye si mtu wa kuficha hisia zake.

Musa

KShs7,500.00
Musa Kibaya anatimuliwa kutoka shule yake ya sita. Anahisi kwamba hii ni rekodi katika umri wake wa miaka kumi na mitano pekee, ingawa kwa namna fulani anaionea fahari. Hofu yake tu ni jinsi Mjomba wake, Silasi, atakavyolichukulia suala hili... n nSilasi anapogundua kutimuliwa kwake, anampeleka Musa katika shule yake ya saba, Mukibi's Educational Institute for the Sons of African Gentlemen. Kumbe, hapo ndipo vituko vya Musa vinapoanza. nMusa ni kitabu cha kwanza katika msururu wa Visa na Vituko vya Musa, vilivyoandikwa na Barbara Kimenye.