Showing 1–20 of 91 results

Maisha ya Mwanaharamu by BENSON MUGO

KShs550.00
Maisha ya Mwanaharamu ni riwaya inayosimulia kisa cha kijana mmoja anayezaliwa nje ya ndoa. Hii ni kulingana na mtazamo wa wanakijiji cha Deka. Kijana huyu anachukuliwa kama mlaanifu na anachukiwa na takribani kila mja katika kijiji hiki. Madhila anayoyapitia yanasababisha afe moyo hivi kwamba anaamua kujitia kitanzi katika Msitu wa Aguzi lakini Ibra, Mungu wa Kijiji cha Deka, anayaokoa maisha yake.

NIZIKWE KWETU KIAMBONI by BENSON MUGO

KShs600.00
Nizikwe Kwetu Kiamboni ni riwaya inayochambua na kufafanua kwa undani madhila yanayoikumba nchi ya Kafila inayoongozwa na kiongozi aliye na uroho wa kutwaa mali yote ya nchi hiyo.

Ninaapa Kwamba(I Solemnly Swear) by L...

KShs1,200.00
Rais Abubakar Bunende wa Jamhuri ya Watu wa Stanza anakula kiapo cha kuwa Rais na kuwahakikishia kuwa wakati huu serikali ya Stanza itasimama kidete kutetea rasilimali za Stanza kuwanufaisha wananchi waliogubikwa na wimbi kubwa la umaskini. Bunende anaamua kubadili baadhi ya sera na mifumo ili kutekeleza azma hiyo lakini anakuja kugundua mambo siyo rahisi hivyo alivyofikiria kwani anakutana na upinzani mzito wa ndani na nje kuzuia hayo anayotaka kufanya kwa sababu yanaingilia maslahi yao. Bunende anapojaribu kutaka kushindana nao wanamuua. Makamu wa Rais Bi. Mai Fabiola anachukua nchi huku akitaka kuendeleza sera za mtangulizi wake nae anafanyiwa jaribio la kuuawawa. Haamini, anachanganyikiwa. Afisa mmoja mwanamama wa Usalama wa Taifa aitwaye Hidaya anaamua kuingia mbele na kutafuta nini mzizi wa mauaji ya Rais Bunende na jaribio la Rais Mai. Nani anahusika ili ammalize.

Chochoro Za Madaraka(Alleys of Power)...

KShs1,200.00
Jasusi na Mwanadiplomasia nguli Joseph Kaduma ama Joe kama alivyozoeleka kuitwa akishirikiana na wenzake wanafanikiwa kumtoa madarakani Rais Sylvester Costa na hivyo kumweka mmoja wa mwenzao kuwa Rais wa Stanza, Habib Chamchua. Lakini hali inageuka kuwa tofauti na walivyokusudia, Korea Kaskazini nchi waliyoitumia kuwasaidia kutimiza azma ile ya kumtoa Rais Costa madarakani wanakuja na matakwa mazito yasiyotekelezeka.Joe na Rais Habib wanakuwa katika wakati mgumu wa ama kutekeleza takwa lile ama kuingia uadui na Korea Kaskazini. Wanaamua kutokutekeleza na hivyo kuingia kwenye msuguano mzito na Korea Kaskazini. Hali inakuwa ya sintofahamu kubwa hadi kupelekea Rais Habib kupotea Ikulu. Ni mtafutano usio wa kawaida.

UJASIRI by Mayfair Wanja

KShs700.00 KShs550.00
It's a Kiswahili story highlighting the many challenges which the boy child/men go through but through courage and determination they overcome them and become successful in life

Sauti Za Washairi by Matata Hassan

KShs700.00 KShs550.00
Diwani hii ni kamilifu katika kukuza lugha ya mwanafunzi pamoja na kumtayarisha katika mtihani wake wa kitaifa. Ndani ya diwani hii, mwanafunzi atakumbana na maelekezo kamili kama vile Sifa mbali mbali za mashairi, bahari, jinsi ya kuutumia Uhuru wa mshairi, Pasona/nafsi neni, lugha ya nadhari na mengine mengi. Fauka ya hayo, mwanafunzi pia atakumbana na maswali na majibu ya mtihani wa kidato cha nne yatakayomsaidia katika kujiweka tayari na mtihani huo. Kwa kifupi, diwani hii ni chombo tosha kinachostahili kuabiriwa sio na mwanafunzi tu bali hata mwalimu anayepania kuwatayarisha wanafunzi vilivyo.

Kichala cha Ushairi by Nickson Hamisi

KShs630.00 KShs599.00
Kichala cha Ushairi kimeshughulikia BAHARI na AINA zote za mashairi na pia kimeshughulikia maswali yote ya mitihani ya KITAIFA KCSE kwanzia mwaka 2007-2023 na mwongozo wake.

Kambi Ya Shetani by Edmond Ongeri

KShs450.00 KShs400.00
Kambi Ya Shetani ni Tamthilia inayozungumzia uozo katika jamii.

Tembe Kajimezea

KShs1,000.00 KShs800.00
“Waonekana mahiri wa lugha na mwenye busara katika kujibu maswali. Majina yako kamili waitwa nani?”, akaniuliza. Mara hii niliweza kuona tabasabu usoni mwake. “Kwa majina naitwa Kazamoyo Juma”, nikamjibu. Uso wake uling’aa mara moja. Sikujua ni kwa nini. Kwani alifahamu jina langu? Nikawaza. “Kazamoyo…kaza…Moyo. Unatoka wapi?”, akaniuliza bwana yule. “Nimetoka kaunti ya Hesabika mjini Weusisi”, nikamjibu. Bwana yule aliruka kutoka kwenye kiti chake na kunikumbatia. Machozi yalimdondoka. Alikuwa amenifahamu. Alikuwa binamu yangu Taru. Katika harakati hiyo niliweza kujiwa na fahamu zangu na kujua kuwa wakati wangu ulikuwa umewadia. Kumbe kutoka siku ile aliponipa kazi katika kampuni yake alikuwa hajanifahamu? Sadfa ilikuwa imetukutanisha.

Mwanzo wa Mwisho na Mwarabu Omari Mwa...

KShs449.00 KShs399.00
Kwikwi za vilio vya bi harusi zinasikika kwa mbali. Kalazimishwa kuwa mke wa mtu, ndoto yake imevunjwa na kusagwasagwa bila ya huruma. Kavalishwa gauni la kiyombo, kichwani katundikwa taji la leso lililopachikwa viwangwa vinavyong`aa. Machozi yanamtoka machoni na kuuharibu wanja aliopakwa. Naam machozi. Si machozi ya furaha bali ya karaha. Binti wa miaka kumi na mitatu hatimaye anaenda kufunga ndoa na mzee wa miaka tisini. Je huu ni mwisho wa ndoto yake Bi harusi aliyoiwekeza toka angali kinda? Ama ndio mwanzo wa shida zake kuisha? Mwanzo wa Mwisho ni riwaya iliyojikita nchini Fokota. Wanawake wa jamii hii wametengwa na kudharaulika. Wao hawana kauli mbele ya wanaume. Mateso, binti aliyekulia kwenye utandabui wa unyanyapaa alijikusuru kuing`oa mizizi hiyo. Je atakumbana na yepi njiani? Na je atafaulu? Mwarabu Omari Mwarabu ni mwandishi anayechipuka kwa kasi mno kwenye sanaa ya utunzi wa hadithi za kiswahili. Alizaliwa Bodo, Kaunti ya Kwale mwaka wa 2000. Mwanzo wa Mwisho ni riwaya yake ya pili baada ya ile ya kwanza iitwayo Daraja la Mauti. Kwa sasa ni mwanafunzi wa chuo kikuu cha Rongo , anasomea Shahada ya Takwimu na Tarakilishi. Pia ni mwanachama wa CHAWAKAMA Kenya.

Arusi Tatu na Wilson Ireri

KShs649.00 KShs499.00
Arusi Tatu Arusi tatu ni simulizi inayotuchorea picha kamili ya safari ya mwanadamu. Wepesi na ugumu wa safari hizo umeelezwa kwa ubatini katika maana kamili ya 'Arusi Tatu'. Mwandishi Wilson Ireri anatusafirisha katika safari ya vijana watatu wenye hulka baidi kama ardhi na mbingu. Wa kwanza Shida ana shida kama lilivyo jina lake. Alichorithi kutoka kwa wazaziwe ni shida tu. Je, atapiga mbizi vipi katika bahari yenye mawimbi ya ufukara ili aufikie ufuo wa ufanisi? Daniel na Don ni pacha hawa hawajui shida ni nini. Wamelelewa katika maisha ya tunu na tamasha. Je neema waliyo nayo wataitumia kuijenga kesho yao? Mwisho mwandishi anatuelewesha kuwa kila mtu ana kipawa chake..." Ni shida ipi inayotokea mtu asipojua kipawa chake? Wilson Ireri ni mwandishi wa hadithi fupi, riwaya na mashairi. Kwa sasa Wilson ni Kasisi katika Dayosisi ya Mlima Kenya Magharibi kanisa la Kianglikana.

Nizike Sijafa na Darius Makhoka

KShs549.00 KShs449.00
Hadithi hii ya Nizike Sijafa ina mnato na mvuto wa aina yake, imekolezwa uhalisia wa maisha katika siku hizi na dunia ya sasa. Mwandishi anasimulia jinsi mwanadamu anavyothamini mfu na kuyapa hadhi kubwa maziko kinyume na anavyomtunza na kumthamini mwenzake awapo hai. Je, Salama Makori atafaulu katika azimio lake la kuihamasisha jamii kuikumbatia methali isemayo udugu ni kufaana wala si kufanana? Je, Salama atapata afueni na kuishi maisha yenye furaha, licha ya umasikini wa sina sinani unaomwandama na kutishia kulizamisha dau la matumaini yake kila uchao? Soma ufaidi! * Mwandishi wa kazi hii ni Darius Makokha. Darius Makokha ni mwandishi ambaye ameibuka kuwa stadi mno katika sanaa ya utunzi wa hadithi za Kiswahili. Halima Apaa Angani na Nizike Sijafa ni mojawapo ya kazi ambazo amezikamilisha. Kwa sasa ni mwalimu wa somo la Kiswahili katika shule tajika ya Mekaela Likunda, mojawapo ya shule za Mekaela Academies – Kwale.

Kudra na Kevin Oyugi

KShs769.00 KShs649.00
Riwaya hii ya Kudra ni ya aina yake. Ni riwaya ambayo imeyamulika masuala ya kisasa na yanayoiathiri jamii kwa njia hasi ama chanya. Mhusika Kudra anajipata akitopea katika ukwasi wa aina yake licha ya kuzaliwa katika jamii ya ukata hohehahe. Hizi zinakuwa ni kudra za Mwenyezi Mungu au majaaliwa kama waambavyo wengine. Mbali na haya majaaliwa yake, anafikwa na mkosi pale ambapo rafiki yake wa chanda na pete Jane anafia katika chumba chake. Hii ni baada ya wao kulewa chopi na kusindikizwa kiamboni kwa Kudra na Bwana Majuto usiku uliotangulia. Je, haya ni majaaliwa pia? Kakaye Kudra, Oscar Mpimbi naye katika umasikini wake anafanikiwa kuchumbiana na Daktari Agnes aliyekuwa akimtibu mamaye kabla ya kuaga dunia. Oscar anampenda Agnes licha ya kuogopa kumjuvya hali ya hisia zake. Kwa upande mwingine, Agnes naye anampenda Oscar na kuamua kumfahamisha. Je, hii ni kudra ya Rabana pia? Utamu wa riwaya hii hauishii tu kuisoma kwa burudani ila pia kujifunza masuala ibuka na ainati katika jamii. Ni riwaya ya kizazi cha leo na uleo ndani mwake! Jipatie nakala ujifahamishe zaidi!

Pandashuka By Timothy O. Sumba

KShs649.00 KShs600.00
“Nikumbukapo mashaka tipitipi yaliyoizonga familia yetu naamini kuwa ulimwengu umefurika malimwengu ya kila nui ambayo hukingama mbele ya walimwengu maishani na kusababisha pandashuka. Kama barabara ndefu ilivyo safari ya Maisha haikosi mabonde, vilima, milima, tambarare na kona. Je. Ni gurufu gani isiyokuwa na gurufu? Kwa bahati njema mawimbi ya safari ngumu hayadumu maishani, huisha namna Maisha yenyewe yanavyoisha. Baadhi ya Pandashuka ni furaha na huzuni, raha karaha, vicheko na vilio, utajiri na umaskini, shibe na njaa, amani na vita, afya njema na maradhi, upendo na chuki n ahata shwari na shari namna wasemavyo wengine. Kimsingi, pandashuka hutusambazia ama utulivu au uchungu nzima unaozaa jakomoyo sufufu. Je, ni nani asiyejua kuwa painamapo ndipo painukapo?” "Ni riwaya ya kitawasifu inayomfahamisha msomaji kutalii katika usimulizi aula uliosukwa kwamba ni mlo wa kisanaa kwa kukolezwa mbinu kemkem za sanaa. Mwandishi aliyetopia na kugharika ukwasi wa lugha ameyatumia maneno ya kawaida namna isiyo ya kawaida ili kuukamilisha ubunifu usio na kifani. Mwandishi huyu mahiri amesimulia visa tele vinavyoingiliana na kuunda taswira halisi za pandashuka katika jamii..." Tahakiki ya Fatma Ali Mohamed(Zanzibar)

Adhabu Ya Maisha By Elishaphan Wachira

KShs500.00 KShs449.00
Mwaisambe alipata taarifa kwamba katika jimbo lao la Matusitusi kulikuwako na mganga mashuhuri. Mganga huyo aliwatibu watu kwa dawa za kienyeji alizokuwa nazo daima. Basi baada ya kusikia habari kumhusu mganga huyo, Mwaisambe aliamua kwenda kumtembelea. Ndugu Mwaisambe anaonekana kuishi maisha ya kubahatisha. Ni mfano wa vijana wanaoonekana kukosa ruwaza, wanabebwa hobelahobela na upepo wa nakama na kuwaangamiza. Mwaisambe yu safarini kumtafuta mganga mashuhuri asiyemjua asili wala fasili yake. Anapanda milima na kuivuka miamba hadi katika eneo la Kivunja Kimya. Atafaulu kumpata mganga wake? Jisomee upate kujua… * Bwana Elishaphan Wachira ni miongoni mwa waandishi wanaochipuka kwa kasi sana. Anajikusuru daima kuandika kwa lugha ya Kiswahili na kukiendeleza. Kwa sasa ni mwalimu wa Kiswahili katika shule ya upili ya Wasichana ya Rarakwa katika Gatuzi la Murang’a. Anajaribu kwa udi na uvumba kukiendeleza Kiswahili kupitia kazi bunilizi. Kwa sasa anamiliki shahada ya ualimu kutoka Chuo Kikuu cha Kenyatta.

Kengeza La Jasiri By Shisia Wasilwa

KShs749.00 KShs699.00
Jasiri ana Kengeza. Kengeza hilo halimpi amani. Linamsumbua maishani. Hilo kengeza linayaunganisha maisha yake ya zamani na usasa. Kalipata ujanani. Amekataa kulizika katika kaburi la sahau. Je, Jasiri atapata tiba ya kengeza hilo analopenda, kulificha pembeni mwa kijoyo chake? Anagundua pia marehemu babake kaaga dunia kutokana na hilo kengeza. Je, haya makengeza ndiyo nini? Ni masimulizi yanayonata, yaliyosheheni taharuki na maudhui mazito. Kuhusu mwandishi Shisia Wasilwa ni mwandishi na mwanahabari stadi wa siku nyingi. Aliwahi kuhudumu na Shirika la Habari nchini Kenya-KBC, China Radio Kimataifa, Citizen Tv na Radio, BBC na Deutsche Welle-DW. Baadhi ya kazi zake ni pamoja Makovu ya Uhai na Dunia Tambara Bovu. Alihariri Ndoto ya Almasi chake Ken Walibora, mwongozo wa Utengano wa Said. A. Mohammed miongoni mwa kazi nyingine teule. Kwa sasa anazamia shahada ya uzamili katika masuala ya mawasiliano katika chuo Kikuu cha Aga Khan.

Walanyama na Mashairi Mengine by Ken ...

KShs800.00 KShs650.00
WALANYAMA ni diwani la mashairi yanayoonyesha taswira ya jamii ya sasa. Jamii ambayo imetawaliwa na dhulma, unyanyasaji, unafiki na jinsi mapenzi yamekosa maana kwa kuyapuuza maswala ya jadi. WALANYAMA ni nyenzo ya bahari mbalimbali za ushairi zilizoshughulikiwa kwa ukamilifu kwa manufaa ya jamii yote ya ulimwengu.

Nyumba Ya Msonge Ya Nyanya Yangu

KShs300.00 KShs230.00
Title: Nyumba ya Msonge ya Nyanya Yangu Series: Msururu wa Discovery Author: Toroitich Patrick Yegon Target Class: Early Readers grade 1-3 Hadithi hii inalenga kukuza uelewa wa watoto wa mazingira yao na kuwawezesha kutunga hadithi kuhusu vifaa, wanyama, maliasili na vitu vingine vingi wanoatumia kila siku. Hadithi hii imeandikwa kulingana na maisha ya kijijini. Inazungumza kuhusu maisha yake nyanya ya msimulizi na jinsi anavyoishi na wanajamii wengine, marafiki, wageni na pia wanyama wao.

Likizo Mashambani by Toroitich Patric...

KShs500.00 KShs350.00
Title: Likizo Mashambani Series: Hadithi za Kiafrika Author: Toroitich Patrick Yegon Target Readers: Class 5,6,7,8 Hadithi hii inasimulia matukio aliyoyapitia Shani alipozuru kijijini Kaplelekwo wakati wa likizo ya Aprili. Katu Maishani Shani hakuwahi kutarajia kuwa angewahi lia kwa kuondoka Kaplelekwo kama alivyofanya siku hiyo alipokuwa akienda kuabiri gari lililokuwa likimngoja.