Showing 1–20 of 27 results

Tembe Kajimezea

KShs1,000.00 KShs800.00
“Waonekana mahiri wa lugha na mwenye busara katika kujibu maswali. Majina yako kamili waitwa nani?”, akaniuliza. Mara hii niliweza kuona tabasabu usoni mwake. “Kwa majina naitwa Kazamoyo Juma”, nikamjibu. Uso wake uling’aa mara moja. Sikujua ni kwa nini. Kwani alifahamu jina langu? Nikawaza. “Kazamoyo…kaza…Moyo. Unatoka wapi?”, akaniuliza bwana yule. “Nimetoka kaunti ya Hesabika mjini Weusisi”, nikamjibu. Bwana yule aliruka kutoka kwenye kiti chake na kunikumbatia. Machozi yalimdondoka. Alikuwa amenifahamu. Alikuwa binamu yangu Taru. Katika harakati hiyo niliweza kujiwa na fahamu zangu na kujua kuwa wakati wangu ulikuwa umewadia. Kumbe kutoka siku ile aliponipa kazi katika kampuni yake alikuwa hajanifahamu? Sadfa ilikuwa imetukutanisha.

Mwanzo wa Mwisho na Mwarabu Omari Mwa...

KShs449.00 KShs399.00
Kwikwi za vilio vya bi harusi zinasikika kwa mbali. Kalazimishwa kuwa mke wa mtu, ndoto yake imevunjwa na kusagwasagwa bila ya huruma. Kavalishwa gauni la kiyombo, kichwani katundikwa taji la leso lililopachikwa viwangwa vinavyong`aa. Machozi yanamtoka machoni na kuuharibu wanja aliopakwa. Naam machozi. Si machozi ya furaha bali ya karaha. Binti wa miaka kumi na mitatu hatimaye anaenda kufunga ndoa na mzee wa miaka tisini. Je huu ni mwisho wa ndoto yake Bi harusi aliyoiwekeza toka angali kinda? Ama ndio mwanzo wa shida zake kuisha? Mwanzo wa Mwisho ni riwaya iliyojikita nchini Fokota. Wanawake wa jamii hii wametengwa na kudharaulika. Wao hawana kauli mbele ya wanaume. Mateso, binti aliyekulia kwenye utandabui wa unyanyapaa alijikusuru kuing`oa mizizi hiyo. Je atakumbana na yepi njiani? Na je atafaulu? Mwarabu Omari Mwarabu ni mwandishi anayechipuka kwa kasi mno kwenye sanaa ya utunzi wa hadithi za kiswahili. Alizaliwa Bodo, Kaunti ya Kwale mwaka wa 2000. Mwanzo wa Mwisho ni riwaya yake ya pili baada ya ile ya kwanza iitwayo Daraja la Mauti. Kwa sasa ni mwanafunzi wa chuo kikuu cha Rongo , anasomea Shahada ya Takwimu na Tarakilishi. Pia ni mwanachama wa CHAWAKAMA Kenya.

Arusi Tatu na Wilson Ireri

KShs649.00 KShs499.00
Arusi Tatu Arusi tatu ni simulizi inayotuchorea picha kamili ya safari ya mwanadamu. Wepesi na ugumu wa safari hizo umeelezwa kwa ubatini katika maana kamili ya 'Arusi Tatu'. Mwandishi Wilson Ireri anatusafirisha katika safari ya vijana watatu wenye hulka baidi kama ardhi na mbingu. Wa kwanza Shida ana shida kama lilivyo jina lake. Alichorithi kutoka kwa wazaziwe ni shida tu. Je, atapiga mbizi vipi katika bahari yenye mawimbi ya ufukara ili aufikie ufuo wa ufanisi? Daniel na Don ni pacha hawa hawajui shida ni nini. Wamelelewa katika maisha ya tunu na tamasha. Je neema waliyo nayo wataitumia kuijenga kesho yao? Mwisho mwandishi anatuelewesha kuwa kila mtu ana kipawa chake..." Ni shida ipi inayotokea mtu asipojua kipawa chake? Wilson Ireri ni mwandishi wa hadithi fupi, riwaya na mashairi. Kwa sasa Wilson ni Kasisi katika Dayosisi ya Mlima Kenya Magharibi kanisa la Kianglikana.

Nizike Sijafa na Darius Makhoka

KShs549.00 KShs449.00
Hadithi hii ya Nizike Sijafa ina mnato na mvuto wa aina yake, imekolezwa uhalisia wa maisha katika siku hizi na dunia ya sasa. Mwandishi anasimulia jinsi mwanadamu anavyothamini mfu na kuyapa hadhi kubwa maziko kinyume na anavyomtunza na kumthamini mwenzake awapo hai. Je, Salama Makori atafaulu katika azimio lake la kuihamasisha jamii kuikumbatia methali isemayo udugu ni kufaana wala si kufanana? Je, Salama atapata afueni na kuishi maisha yenye furaha, licha ya umasikini wa sina sinani unaomwandama na kutishia kulizamisha dau la matumaini yake kila uchao? Soma ufaidi! * Mwandishi wa kazi hii ni Darius Makokha. Darius Makokha ni mwandishi ambaye ameibuka kuwa stadi mno katika sanaa ya utunzi wa hadithi za Kiswahili. Halima Apaa Angani na Nizike Sijafa ni mojawapo ya kazi ambazo amezikamilisha. Kwa sasa ni mwalimu wa somo la Kiswahili katika shule tajika ya Mekaela Likunda, mojawapo ya shule za Mekaela Academies – Kwale.

Kudra na Kevin Oyugi

KShs769.00 KShs649.00
Riwaya hii ya Kudra ni ya aina yake. Ni riwaya ambayo imeyamulika masuala ya kisasa na yanayoiathiri jamii kwa njia hasi ama chanya. Mhusika Kudra anajipata akitopea katika ukwasi wa aina yake licha ya kuzaliwa katika jamii ya ukata hohehahe. Hizi zinakuwa ni kudra za Mwenyezi Mungu au majaaliwa kama waambavyo wengine. Mbali na haya majaaliwa yake, anafikwa na mkosi pale ambapo rafiki yake wa chanda na pete Jane anafia katika chumba chake. Hii ni baada ya wao kulewa chopi na kusindikizwa kiamboni kwa Kudra na Bwana Majuto usiku uliotangulia. Je, haya ni majaaliwa pia? Kakaye Kudra, Oscar Mpimbi naye katika umasikini wake anafanikiwa kuchumbiana na Daktari Agnes aliyekuwa akimtibu mamaye kabla ya kuaga dunia. Oscar anampenda Agnes licha ya kuogopa kumjuvya hali ya hisia zake. Kwa upande mwingine, Agnes naye anampenda Oscar na kuamua kumfahamisha. Je, hii ni kudra ya Rabana pia? Utamu wa riwaya hii hauishii tu kuisoma kwa burudani ila pia kujifunza masuala ibuka na ainati katika jamii. Ni riwaya ya kizazi cha leo na uleo ndani mwake! Jipatie nakala ujifahamishe zaidi!

Pandashuka By Timothy O. Sumba

KShs649.00 KShs600.00
“Nikumbukapo mashaka tipitipi yaliyoizonga familia yetu naamini kuwa ulimwengu umefurika malimwengu ya kila nui ambayo hukingama mbele ya walimwengu maishani na kusababisha pandashuka. Kama barabara ndefu ilivyo safari ya Maisha haikosi mabonde, vilima, milima, tambarare na kona. Je. Ni gurufu gani isiyokuwa na gurufu? Kwa bahati njema mawimbi ya safari ngumu hayadumu maishani, huisha namna Maisha yenyewe yanavyoisha. Baadhi ya Pandashuka ni furaha na huzuni, raha karaha, vicheko na vilio, utajiri na umaskini, shibe na njaa, amani na vita, afya njema na maradhi, upendo na chuki n ahata shwari na shari namna wasemavyo wengine. Kimsingi, pandashuka hutusambazia ama utulivu au uchungu nzima unaozaa jakomoyo sufufu. Je, ni nani asiyejua kuwa painamapo ndipo painukapo?” "Ni riwaya ya kitawasifu inayomfahamisha msomaji kutalii katika usimulizi aula uliosukwa kwamba ni mlo wa kisanaa kwa kukolezwa mbinu kemkem za sanaa. Mwandishi aliyetopia na kugharika ukwasi wa lugha ameyatumia maneno ya kawaida namna isiyo ya kawaida ili kuukamilisha ubunifu usio na kifani. Mwandishi huyu mahiri amesimulia visa tele vinavyoingiliana na kuunda taswira halisi za pandashuka katika jamii..." Tahakiki ya Fatma Ali Mohamed(Zanzibar)

Adhabu Ya Maisha By Elishaphan Wachira

KShs500.00 KShs449.00
Mwaisambe alipata taarifa kwamba katika jimbo lao la Matusitusi kulikuwako na mganga mashuhuri. Mganga huyo aliwatibu watu kwa dawa za kienyeji alizokuwa nazo daima. Basi baada ya kusikia habari kumhusu mganga huyo, Mwaisambe aliamua kwenda kumtembelea. Ndugu Mwaisambe anaonekana kuishi maisha ya kubahatisha. Ni mfano wa vijana wanaoonekana kukosa ruwaza, wanabebwa hobelahobela na upepo wa nakama na kuwaangamiza. Mwaisambe yu safarini kumtafuta mganga mashuhuri asiyemjua asili wala fasili yake. Anapanda milima na kuivuka miamba hadi katika eneo la Kivunja Kimya. Atafaulu kumpata mganga wake? Jisomee upate kujua… * Bwana Elishaphan Wachira ni miongoni mwa waandishi wanaochipuka kwa kasi sana. Anajikusuru daima kuandika kwa lugha ya Kiswahili na kukiendeleza. Kwa sasa ni mwalimu wa Kiswahili katika shule ya upili ya Wasichana ya Rarakwa katika Gatuzi la Murang’a. Anajaribu kwa udi na uvumba kukiendeleza Kiswahili kupitia kazi bunilizi. Kwa sasa anamiliki shahada ya ualimu kutoka Chuo Kikuu cha Kenyatta.

Kengeza La Jasiri By Shisia Wasilwa

KShs749.00 KShs699.00
Jasiri ana Kengeza. Kengeza hilo halimpi amani. Linamsumbua maishani. Hilo kengeza linayaunganisha maisha yake ya zamani na usasa. Kalipata ujanani. Amekataa kulizika katika kaburi la sahau. Je, Jasiri atapata tiba ya kengeza hilo analopenda, kulificha pembeni mwa kijoyo chake? Anagundua pia marehemu babake kaaga dunia kutokana na hilo kengeza. Je, haya makengeza ndiyo nini? Ni masimulizi yanayonata, yaliyosheheni taharuki na maudhui mazito. Kuhusu mwandishi Shisia Wasilwa ni mwandishi na mwanahabari stadi wa siku nyingi. Aliwahi kuhudumu na Shirika la Habari nchini Kenya-KBC, China Radio Kimataifa, Citizen Tv na Radio, BBC na Deutsche Welle-DW. Baadhi ya kazi zake ni pamoja Makovu ya Uhai na Dunia Tambara Bovu. Alihariri Ndoto ya Almasi chake Ken Walibora, mwongozo wa Utengano wa Said. A. Mohammed miongoni mwa kazi nyingine teule. Kwa sasa anazamia shahada ya uzamili katika masuala ya mawasiliano katika chuo Kikuu cha Aga Khan.