Showing all 2 results

Tunu ya Ushairi

KShs8,500.00
Tunu ya Ushairi ni mkusanyo wa mashairi ya aina, maudhui na mitindo mbalimbali. Kuna mashairi arudhi, mashairi huru na mashairi picha. Diwani hii ina mashairi ambayo msomaji atajihusisha nayo kwa njia rahisi. Ujumbe wake unapitishwa kwa njia sahili na yenye mguso unaoiacha athari ya kudumu kwa msomaji. Washairi hawakujikita katika mikondo iliyopo tu; wamezuka na mikondo mipya ya utungaji wa mashairi arudhi ambayo itachangia kubadilisha mtazamo wetu kuhusu aina za mashairi. Mkusanyo huu unatoa changamoto kwa wahakiki wa fasihi kutathmini upya upya maelezo dhana mbalimbali za ushairi.

Fani ya Fasihi Simulizi kwa shule za ...

KShs825.00
'Fani ya Fasihi Simulizi' kwa Shule za Upili kimeandikwa kwa lengo la kumfafanulia mwanafunzi tanzu na vipera vya fasihi simulizi kwa njia angavu na nyepesi. nMahitaji yote ya silabasi ya shule za upili yameshughulikiwa kwa kina. nMada zimejadiliwa kwa lugha rahisi na mifano anuwai ya uchanganuzi kutolewa. nYapo maswali yaliyotolewa mwishoni mwa mada. Maswali haya yanatahini stadi zote za ufumbuzi. Mwishoni mwa kitabu kumetolewa majibu ya baadhi ya maswali ya mazoezi. n nAssumpta K Matei ni mwalimu mwenye tajriba pana katika ufundishaji wa Kiswahili. Pia ameandika vitabu kadha vya kufunzia lugha na fasihi ya Kiswahili.