Showing all 11 results

Wasakatonge

KShs6,500.00
Wasakatonge ni diwani yake mpya yenye hazina ya mashairi yenye kubainisha sauti kali ya utetezi kwa wavujajasho wanaonyanyaswa, kuonewa, kudharauliwa na kunyonywa nguvu zao. Ni kauli inayobainisha uoza wa jamii na athari zake kwa wanyonge. Diwani hii ni chachu ya kuuzindua umma ulioghilibiwa iii udai haki yao dhidi ya wanasiasa madikteta wanaotumia nguvu za dola kwa maslahi yao. n
    n
  • Kitabu hiki mbali ya kuwa na kina kizito cha maudhui, fani yake pia imetia fora. Kwa wale wapendao ushairi "bulibuli" wa Kiswahili hiki ndicho kitabu chao. Wanafunzi wa sekondari, vyuo na vyuo vikuu watafaidika sana wasomapo diwani hii.
  • n
  • Mwishoni mwa kitabu hiki, kuna orodha ndefu ya maneno na maana yake ambayo bila shaka yatakuwa hazina kubwa katika kuyafaidi na kuyaelewa ipasavyo mashairi haya.
  • n

Tubadilishe Jina

KShs8,500.00
Kinyume na sifa na siha yake, kaunti aliyoitawala ilikuwa nyeusi; weusi uliowatia wakazi huzuni kutokana na ulafi na mapuuza ya viongozi. Baya zaidi, sauti za wapinzani dhidi ya umaskini, ukosefu wa ajira na magonjwa zilizimwa. Tubadilishe Jina ni riwaya inayomulika maovu mbalimbali katika jamii yetu ya leo, na madhara yanayotokana na uongozi mbaya. Hadithi hii, vilevile, inaangazia nafasi ya uanaharakati katika kuupiga msasa uongozi ili kudumisha maadili katika jamii.

Sauti ya Dhiki (Toleo Jipya)

KShs7,000.00
Diwani hii - inayosheheni mashairi kuhusu utamaduni, mapenzi, nasaha, siasa, mambo ya kinyumbani, n.k. - ilitungwa baina ya 1969 na 1972 ambapo mtunzi alikuwa kifungoni baada ya kupatikana na hatia ya kuwachochea watu ili waipindue Serikali ya Kenya kwa kutumia silaha. Kwa hivyo, unapoisoma diwani hii hutaweza kujizuia kuona athari ambayo kifungo huweza kuwa nayo kwa mfungwa. n nJambo la maana sana kuhusu diwani hii ni kwamba mtunzi ameweza kuzungumzia mambo ya kisasa, kama alivyofanya katika shairi la 'Usiniuwe!', bila kupotoka na kutafuta mifano ya kigeni. Hili ndilo lililompa Shihabuddin Chiraghdin, mmoja wa wataalamu mashuhuri wa lugha ya Kiswahili, kusema katika utangulizi wake kwamba, ingawa mtunzi ameingiliwa na athari za kigeni kwa ajili ya elimu aliyoipata shuleni, 'hakukubali kuzongwazongwa na athari hizo, hivyo mashairi yake hayana maingilio ya miundo ya kigeni hata chembe, na mawazo yake yote yameambatana na Uswahili na Uafrika kwa jumla'. n nKitabu hiki kitawafaa wale wapendao kusoma mashairi ya Kiswahili ya kiwango cha juu, na vilevile wanafunzi wa fasihi ya Kiswahili katika shule za sekondari na vyuo vikuu.

Passenger 141

KShs6,000.00
Recently there has been a leakage of highly sensitive information and photographs that may damage relations between two nations. Nyutu - code name Stinging Bee - is assigned the task of tracking down the culprit and silencing the source. He has to travel to Mombasa to do this.

The Hunter is Back

KShs6,000.00
Rita is faced with trials that seem to seal her fate. Political power, big money, and betrayal in her family have conspired nto ruin her family forever. After a regrettable past, a stressful present and a clearly bleak future, will she be able to overcome the forces of evil?

Ningekuwa Na Uwezo

KShs7,500.00
Je, ungekuwa na uwezo wa kubadili ulimwengu unamoishi, ungeubadili? Ungebadili nini?

Malenga Wapya

KShs5,500.00
Diwani hii ya "Malenga Wapya" imekusanya mashairi 37 ambayo yana ukwasi mkubwa wa fani na maudhui na yametumia mitindo mbalimbali ya mashairi ya Kiswahili. Malenga wetu hawa wapya wamejitahidi sana kuchora picha ambazo zinaakisi utamaduni wa Kiswahili na waswahili wenyewe. n nMaudhui yaliyotawala katika mashairi haya ni pamoja na maswala ya ukombozi wa mwanamke, uonevu na umasikini, kilimo, ugumu wa maisha, usaliti, uzembe, misiba, mapenzi na demokrasia katika jamii. Mwishoni mwa kitabu hiki kuna orodha ndefu ya maneno na maana yake ambayo bila shaka yatakuwa hazina kubwa katika ufahamu wa mashairi haya. n nVitabu vingine vya mashairi katika mfululizo huu ni: n
    n
  • Malenga wa Mrima
  • n
  • Malenga wa Mvita
  • n
  • Malenga wa Vumba
  • n

Kwenye Ukingo wa Thim

KShs6,000.00
Tamthilia ya "Kwenye Ukingo wa Thim" inaonyesha migogoro iliyopo baina ya mahitaji ya mila na mahitaji ya maisha ya kisasa. Mwandishi amefaulu kuonyesha mvutano huo unavyoweza kutokea na athari zake kwa wanaohusika.

Masaibu Ya Ndugu Jero

KShs7,500.00
Author: Wole Soyinka ISBN: “9780195722451”

The Trials of Brother Jero

KShs7,500.00
Brother Jeroboam is a self-professed man of God who preaches water but drinks wine. He has managed to convince a group of people that he is God's prophet with divine powers to have their dreams fulfilled. Through this, he takes advantage of his faithful who are just too eager to be told what they want to hear. Like many of the 'prophets', we see everywhere today, Brother Jero, as he likes to be called, has managed to keep his followers in a tight grip of spiritual slavery. When Chume, his faithful assistant and heir apparent, discovers the real man behind the mask, Brother Jero won't stop at anything to make sure that he is 'well taken care of'!

Kinjeketile (Kiswahili)

KShs11,000.00
Author: Ebrahim Hussein ISBN: “9780195720297”