Old Money

KShs10,500.00
Rita, the ambitious matriarch of the Mugambi empire, is an overbearing mother to her sons, Zain and Bahati. She runs her family as she runs her businesses – with an iron fist - and swiftly and mercilessly deals with any sign of rebellion. Are the boys willing to sacrifice their fortunes and status for the sake of freedom and a chance to reinvent themselves? n nSet in the dynamic city of Nairobi, Old Money juxtaposes the lives of those privileged to be sitting in the lap of luxury, with the lives of those eking out a living. The author draws us into a deeply riveting journey of transformation which explores corruption, exploitation, family relationships and blind ambition.

Msako Hatari

KShs8,000.00
Inaichukua idara ya polisi zaidi ya miaka miwili bila kubaini chanzo wala sababu ya kuuawa kwa Mzee Majoro na mkewe, hali inayomtia mwanano Jackline wasiwasi mkubwa. Katika kutafuta haki, Jackline anamshirikisha mpelelezi Daniel Mwaseba kwenye harakati hizo, japo kwa siri. Uchunguzi wa Daniel unahusisha vifo hivyo na faili fulani ambalo limesababisha pia vifo na mateso kwa kila anayehusika kulisaka. Je, faili lenyewe lina nini? Je, Daniel atafanikisha msako huo uliowashinda hata wakuu wa polisi? n nMsako Hatari ni kisa cha kijasusi kilichosukwa kwa upekee usio mfano. Mbali na kuwa kinaangazia maovu na udhalimu katika jamii, kinatoa mafunzo chungu nzima kuhusu haki na maadili.

Mashaka

KShs5,500.00
Nini ambacho Kiburi hakubarikiwa nacho; mali, ulimbwende au umaarufu? Lakini, vyote hivi havikutosha kumpa raha aliyoisaka maishani. Kwa upande mwingine, Mashaka anakumbana na mashaka kwa sababu ya kiburi cha Kiburi. Sio kwamba Kiburi hakumpenda Mashaka. La, hasha! Alimpenda sana na alikuwa tayari kumwaga mali yake yote, mradi tu ampate. Basi, binadamu huhitaji nini ili kufurahia ukamilifu wa maisha? Hili ndilo swali ambalo mwandishi anauliza katika kisa hiki cha kuburudisha na kuelimisha.

Waja Leo

KShs7,000.00
"Waja leo" ni mkusanyiko wa mashairi ya aina yake yanayomulikia kurunzi vipengele anuwai vya waja (binadamu) wa leo. Watunzi wa mashairi katika diwani hii wana tajiriba na falsafa tofautitofauti zinazodhihirishwa na mitindo na maudhui yao mbalimbali. Mashairi yenyewe yameandikwa kwa lugha rahisi kusomeka na kueleweka, yaliyo na mvuto wa ajabu na ambayo yatawafaa wapenzi na wasomi wa mashairi ndani na nje ya mipaka ya asasi za elimu. n nKatika diwani hii, mna utangulizi kwa msomaji wenye maelezo mwafaka kuhusu mbinu ya kuyasoma na kuyachambua mashairi kwa faida ya wasomaji katika shule za upili. Aidha, kuna maswali ya mazoezi kwenye kurasa za mwisho.

Kosa Si Kosa?

KShs7,000.00
Lullu Katanga, mwanafunzi wa uanasheria, anajikuta korokoroni. Akipatikana na hatia, atahukumiwa kifungo bila dhamana. Shahidi wa pekee anayeweza kumsaidia ni mshiriki ambaye ana hatia zake. Je, shahidi huyu atakubali kumsaidia bila mwenyewe kuonekana mkosa?

Dunia Yao

KShs11,000.00
'Dunia Yao' ni riwaya inayothibitisha namna ujasiri wa mwandishi ulivyoimarika kwa kujadili mambo nyeti kuhusu jamii yake na mataifa. Tunakutana na Ndi- anayejifungia njozini kukimbia ukweli unaompa mateso na kuihangaisha akili yake. Mwishowe anaishiwa na kila kitu ila ishara za mauti. Kwa nini? Kitendawili hiki tunakuachia wewe msomaji ukitegue. n nUlimwengu wa riwaya hii na msuko wake, na umbo lake na muundo wake, kamwe si wa kawaida. Umetengenezwa kumvutia msomaji kwa njia ya ajabu. Ni wa majaribio yanayovunja sarufi au kanuni zote za lugha na sanaa ili ufanane na dunia tunayoishi leo. Dunia ambayo ni tata na ovyo, iliyobutuka, iliyoparaganyika, inayotuchezesha foliti za mauti, inayonata utamu wa kifo na uchungu wa uhai. Inamtafuta msomaji imnase mara anapokikamata kitabu.

Kitumbua Kimeingia Mchanga

KShs7,000.00
'Kitumbua Kimeingia Mchanga' ni tamthilia inayozusha mawazo kuhusu tofauti zilizoko baina ya mila na tamaduni za kale na za kisasa kuhusu suala la ndoa. Pia imeshughulikia uhuru wa vijana wa kileo kinyume na matakwa ya wazee wao. Fikirini hakubali kuchaguliwa mke na babake, Bw Mambo na nyanyake, Bi Hoja. Wazee wake wanaona jambo la kumchagulia mtoto wao mke ni jukumu lao. Vilevile, wanamtuhumu Hidaya, msichana ambaye Fikirini anataka kumuoa, kuwa ni kiruka njia, mhuni na muovu. Je, Fikirini atashinda kuwatoa shaka na kuwashawishi wazee wake wamkubalie analolipenda? Je, ndoa ya Fikirini itafanikiwa?