QUICK DELIVERY
Swift dispatch
ONLINE PAYMENT
Multiple options
EXPERT SUPPORT
Help when you need it
WIDE VARIETY
Thousands of books
GLOBAL SHIPPING
Worldwide delivery
0794 233 261
£7.85 £7.25
In stock
Riwaya hii ya Kudra ni ya aina yake. Ni riwaya ambayo imeyamulika masuala ya kisasa na yanayoiathiri jamii kwa njia hasi ama chanya.
Mhusika Kudra anajipata akitopea katika ukwasi wa aina yake licha ya kuzaliwa katika jamii ya ukata hohehahe. Hizi zinakuwa ni kudra za Mwenyezi Mungu au majaaliwa kama waambavyo wengine. Mbali na haya majaaliwa yake, anafikwa na mkosi pale ambapo rafiki yake wa chanda na pete Jane anafia katika chumba chake. Hii ni baada ya wao kulewa chopi na kusindikizwa kiamboni kwa Kudra na Bwana Majuto usiku uliotangulia. Je, haya ni majaaliwa pia?
Kakaye Kudra, Oscar Mpimbi naye katika umasikini wake anafanikiwa kuchumbiana na Daktari Agnes aliyekuwa akimtibu mamaye kabla ya kuaga dunia. Oscar anampenda Agnes licha ya kuogopa kumjuvya hali ya hisia zake. Kwa upande mwingine, Agnes naye anampenda Oscar na kuamua kumfahamisha. Je, hii ni kudra ya Rabana pia?
Utamu wa riwaya hii hauishii tu kuisoma kwa burudani ila pia kujifunza masuala ibuka na ainati katika jamii. Ni riwaya ya kizazi cha leo na uleo ndani mwake! Jipatie nakala ujifahamishe zaidi!
Swift dispatch
Multiple options
Help when you need it
Thousands of books
Worldwide delivery
No account yet?
Create an Account
Reviews
Clear filtersThere are no reviews yet.