Mitego ya Kisasa na Hadithi Nyingine
KShs500.00
Mitego ya Kisasa na Hadithi Nyingine ni mkusanyiko wa hadithi kumi na mbili. Hadithi hizi ni taswira ya hali halisi ya jamii ya kisasa. Antholojia hii imeandikwa kuafiki watu wa umri wowote kutokana na lugha tutumbi iliyotumika pamoja na usahili wa visa hadithini. Ni kazi maridhawa kwa wanafunzi wa sekodari, vyuo vikuu na wenye ari ilhamu ya kujifunza lugha ashirafu ya Kiswahili.
Maudhui aina ainati yameshughulikiwa . Baadhi yao ni; unafiki, wizi, dini, mapenzi na ndoa, ushirikina na mazingaombwe, uongozi mbaya, siasa, nafasi ya vijana na akina mama katika jamii n.k
- Description
- Shipping
- Reviews (0)
- Vendor Info
- More Products
Description
Mitego Kisasa na Hadithi Nyingine ni mkusanyiko wa hadithi fupi unaojumuisha jumla ya hadithi kumi na mbili. Visa vinavyojumuishwa humo ndani ni taswira ya jamii ya sasa. Anthologia hii inaangazia watu wa umri mdogo, wastani na hata wale wazee. Mkusanyiko huu ni madhubuti kwa wanafunzi wa sekodari mwandamizi, vyuo na shule zinazofunza lugha ya Kiswahili. Aidha, mpenzi wa fasihi aliyekita mizizi katika tanzu hio, na yule anayetazamia kujifunza Fasihi Andishi kwa jumla atafaidika pakubwa. Kupitia mkusanyiko huu, utagundua maudhui kama vile: unafiki, wizi, dini, mapenzi, ndoa, uchawi na mazingaombwe, uongozi mbaya ,na nafasi ya vijana na kina mama katika jamii.
Mwandishi amezamia katika mbinu za lugha na kuonyesha jinsi jamii imekumbwa na changamoto nyingi na kuna uwezekano wa kuimarika iwapo matatizo hayo yanasuluhishwa. Kupitia tashtiti na mtindo anuwai, mwandishi anakusudia kuwa utaburudika na kupata mafunzo.
Be the first to review “Mitego ya Kisasa na Hadithi Nyingine”
Vendor Information
- Store Name: Kelvin Munene
- Vendor: Kelvin Munene
-
Address:
chuka street
MEGAVISA
Chuka
Tharaka-Nithi
60400
Kenya - No ratings found yet!
Reviews
There are no reviews yet.