Nimepoteza Tena na Hadithi Nyingine ni mkusanyiko wa hadithi fupi zinazolenga hadhira ya wanafunzi, wasomaji wa kawaida na wataalamu wowote wale. Huu ni mkusanyiko unaowaleta pamoja waandishi walio na viwango vya juu vya ubunifu na ukwasi wa lugha. Hadithi zilizomo kwa ujumla zinagusa nafasi na nafsi ya msomaji. Bila shaka, msomaji yeyote wa mkusanyiko huu atagundua kuwa waandishi wake ni wenye uwezo mkubwa katika utunzi, fauka ya kuwa wengine wao wanalimbukia fasihi andishi. Naam, ulimbukeni wao umeleta sura ngeni katika ulimwengu wa fasihi andishi.
Kikechi Kombo B. ana Shahada ya elimu na sanaa na shahada ya uzamili kutoka Chuo Kikuu cha Kenyatta. Ni mwalimu mwenye tajiriba pana katika lugha na fasihi ya Kiswahili kwa miaka mingi. Hushiriki uchambuzi wa lugha na fasihi katika Idhaa ya Radio Taifa- KBC. Ameandika vitabu vya marudio katika lugha ya Kiswahili na miongozo tolatola mathalan mwongozo wa Chozi la Heri, mwongozo wa Kigogo, mwongozo wa Kidagaa Kimemwozea na mwongozo wa Mstahiki Meya. Amechangia pia katika kitabu cha marudio cha Kioo Cha KCSE, Mwongozo wa Nguu za Jadi na Mapambazuko ya Machweo na hadithi nyingine miongoni mwa vitabu vingine.
Kenna Wasike ni mwandishi wa kazi za fasihi. Ameandika kazi aula za bunilizi. Aidha, amechangia katika uandishi wa hadithi fupi. Hadithi yake maarufu ni ‘Mapenzi ya Kifaurongo’ katika mkusanyiko wa Tumbo Lisiloshiba na Hadithi Nyingine. Vilevile, amechangia katika uandishi wa kitabu cha marudio ya fasihi. Kwa sasa yeye ni mwalimu wa Kiswahili katika Shule ya wavulana ya Chesamisi iliyoko gatuzi la Bungoma nchini Kenya.
Reviews
Clear filtersThere are no reviews yet.