Yananiandama na Hadithi Nyingine ni mkusanyiko wa hadithi fupi zinazolenga hadhira ya wanafunzi, wasomaji wa kawaida na wataalamu wowote wale. Huu ni mkusanyiko unaowaleta pamoja waandishi walio na viwango vya juu vya ubunifu na ukwasi wa lugha. Hadithi zilizomo kwa ujumla zinagusa nafasi na nafsi ya msomaji. Bila shaka, msomaji yeyote wa mkusanyiko huu atagundua kuwa waandishi wake ni wenye uwezo mkubwa katika utunzi, fauka ya kuwa wengine wao wanalimbukia fasihi andishi. Naam, ulimbukeni wao umeleta sura ngeni katika ulimwengu wa fasihi andishi.
Jeff Mandila ni mmoja wa waandishi wanaoinukia kwa kasi mno. Ni mwandishi wa riwaya, tamthilia na hadithi fupi kando na utunzi wa mashairi. Alizaliwa karibu na mji wa Kitale mwaka wa 1985. Alijishindia tuzo ya Wahome Mutahi 2012 baada ya riwaya yake ya Sikitiko la Sambaya kuibuka ya kwanza.
Geoffrey Mung’ou ambaye pia ni mwandishi wa riwaya ya Mkakasi ni mhariri katika Shirika la Habari la Standard. Ana shahada katika kitivo cha Elimu (Kiswahili na Historia-Chuo Kikuu cha Kenyatta). Ametoa mchango mkubwa kuhusu Kiswahili katika vyombo vya habari, kwenye makongamano na shuleni. Aidha, amekuwa mwalimu wa somo la Kiswahili katika shule kadhaa za upili nchini Kenya. Mbali na kazi hizi za fasihi, ameibukia na vitabu adhimu kuhusu fani nyinginezo za lugha.
Reviews
Clear filtersThere are no reviews yet.