QUICK DELIVERY
Swift dispatch
ONLINE PAYMENT
Multiple options
EXPERT SUPPORT
Help when you need it
WIDE VARIETY
Thousands of books
GLOBAL SHIPPING
Worldwide delivery
0794 233 261
KShs700.00
In stock
Dunia imekataa kuwatambua watu kulingana na uwezo na juhudi zao maishani. Mara nyingi tunafumba macho tusibaini kwamba kila mwanadamu amejaliwa talanta ambazo hazitegemei jinsia ya mtu ili kunawiri. Katika riwaya hii ya Talanta si Ndumba, mwandishi ameangazia suala la kutambua uwezo wa binadamu pasi kuegemea kigezo cha jinsia.
Talanta si Ndumba ni riwaya iliyojaa mseto wa matukio ambayo mengine yanaibua hisia za huruma na majuto. Mwinyi Mshaufu anakumbana na vitendawili vya maisha ambapo anafeli kuvitegua! Anajaliwa na watoto wasichana ambao anawaona kama wasiofaa kisa na maana ni wa kike. Mshaufu anajiona kama mzazi aliyefeli na kuamini kwamba kukosa mtoto wa kiume ni sawa na kuishi bila mrithi wa mali na nafasi alizotunukiwa.
Anamfurusha mkewe Siwazuru pamoja na wanawe Mwenge, Lulu na Hariri. Baina ya machozi na rai za wanawe kumwomba baba yao awaonee imani, Mshaufu anashikilia kani kwamba maji kamfika shingoni.
Siwazuru pamoja na wanawe wanakaribishwa na Bibi Nyamwange ambaye anawashauri na kuwapa makao.Wanawe Siwazuru wanatia bidii masomoni na hatimaye kufaulu pakubwa. Talanta zao zinabainika wazi, wanavuma na kujulikana kwingi. Habari hizi zinamfikia baba yao ambaye anazipokea kwa majuto makubwa.
Licha ya mtengo uliozuka, binti zake Mshaufu wanaamua kumsamehe na kuzika tofauti zao. Kwa kweli, kazi hii imejaa mafunzo ainati ambayo lengo lake kubwa ni kumhamasisha msomaji kwamba haifai kumbagua mtu kwa kuzingatia jinsia yake! Kila mtu, wa kike au kiume, ana uwezo sawa!
Swift dispatch
Multiple options
Help when you need it
Thousands of books
Worldwide delivery
No account yet?
Create an Account
Reviews
Clear filtersThere are no reviews yet.