Dkt. KITHAKAWA MBERIA ni mwenyekiti wa Idara ya Isimu na Lugha za Kiafrika, Chuo Kikuu cha Nairobi. Mbali na kusimamia Idara na kufundisha katika nyanja za Kiswahili, isimu na mawasiliano, anajishughulisha na utunzi wa mashairi na tamthilia na pia uchoraji.
Kwa muda mrefu ameshiriki kama mwamuzi katika Tamasha za Muziki za Kenya, Tamasha za Muziki na Utamaduni za Kenya na Tamasha za Uigizaji za Shule na Vyuo za Kenya. Yeye ni mwanakamati wa Kamati ya Kitaifa ya Tamasha za Muziki na Utamaduni za Kenya na vile vile mwanakamati wa Kamati ya Chama cha Waandishi cha Kenya. Vitabu vyake vingine ambavyo vimechapishwa na Marimba Publications Ltd ni Mchezo wa Karata (mashairi) Natala (tamthilia) na
Bara Jingine (mashairi)
Reviews
Clear filtersThere are no reviews yet.