Diwani hii ni kamilifu katika kukuza lugha ya mwanafunzi pamoja na kumtayarisha katika mtihani wake wa kitaifa. Ndani ya diwani hii, mwanafunzi atakumbana na maelekezo kamili kama vile Sifa mbali mbali za mashairi, bahari, jinsi ya kuutumia Uhuru wa mshairi, Pasona/nafsi neni, lugha ya nadhari na mengine mengi.
Fauka ya hayo, mwanafunzi pia atakumbana na maswali na majibu ya mtihani wa kidato cha nne yatakayomsaidia katika kujiweka tayari na mtihani huo. Kwa kifupi, diwani hii ni chombo tosha kinachostahili kuabiriwa sio na mwanafunzi tu bali hata mwalimu anayepania kuwatayarisha wanafunzi vilivyo.