- Mitego ya Kisasa na Hadithi Nyingine ni mkusanyiko wa hadithi kumi na mbili. Hadithi hizi ni taswira ya hali halisi ya jamii ya kisasa. Antholojia hii imeandikwa kuafiki watu wa umri wowote kutokana na lugha tutumbi iliyotumika pamoja na usahili wa visa hadithini. Ni kazi maridhawa kwa wanafunzi wa sekodari, vyuo vikuu na wenye ari ilhamu ya kujifunza lugha ashirafu ya Kiswahili.
Maudhui aina ainati yameshughulikiwa . Baadhi yao ni; unafiki, wizi, dini, mapenzi na ndoa, ushirikina na mazingaombwe, uongozi mbaya, siasa, nafasi ya vijana na akina mama katika jamii n.k