Mwongozo wa Mapambazuko ya Machweo na hadithi nyingine
Waswahili husema cha mwenzako kikinyolewa chako tia maji. Kanseli imebadili mitindo ya utahini nasi sharti tubadili namna ya kuwaelekeza watahiniwa ili chombo kisiende mrama. Maswali ya karne ya 21 yanadhihirisha utahini wa stadi za umahiri na umilisi wa kazi ya fasihi na si kuiga tu kikasuku.
Mitihani ya kitaifa siku hizi inaegemea maswali yanayohitaji uwazaji wa kina, umilisi wa fasihi, usanisi au mbinu telekezi katika nadharia ya Bloom. Maswali ya kale ya maudhui na wasifu wa wahusika hayajitokezi kwa wingi kwani mtihani unalenga ufahamu mpana wa vitushi na msuko na si ufahamu wa kijuu juu tu.
Nakala hii ni mwongozo adhimu na aula kwa mwanafunzi na mwalimu wa shule ya upili kwani inaweka parauwanja maswala mbalimbali kama vile; Umuhimu wa ploti, umuhimu wa mandhari, umuhimu wa usimulizi, mtindo na mwingiliano matini wa vipengele mbalimbali. Nasadiki na kuamini mambo yatatengemea baada ya kupata nakala hii kwani kinolewacho hupata.
Mwandishi ni Shehe Mutwiri mwanafunzi wa shahada ya uzamifu (PhD) na mwalimu mweledi wa Kiswahili anayefahamu mahitaji ya hadhira lengwa
KIMUTAI KIRUI ELISHA –
it’s good and easy understandable
Dama boss –
The stories are so educative