Wema hukuza mema, mikosi na tufani za maisha zilimnyang'anya Stella wazazi. Akajikutamikonono mwa wenyeji walalahoi. Nap wakamuani. Hatua kwa hatua alipanda ngazi kwa usaidizi wa kijana Ombaomba. Akawa awika ndani na nje ya nchi kupitia talanta yake.
Riwaya hii inasimulia vituko vya Biandis katika Jimbo la Aboke, aliyedai kuwa ni walii wa Mungu. Hulka zake lakini zilikiuka kaida za uwalii wa Mungu. Wazee wakabaki kuduwaa.