Novela ya Kaga inaangazia msichana Saida Jitihada ambaye anafikwa na mengi maishani. Hayati baba yake mzazi, Bwana Sanifu Jitihada , mwalimu mashuhuri wa lugha ya Kiswahili anagonga vichwa vya habari kwa usanifu na ubunifu wake. Saida anampoteza mama yake siku ya kutangazwa matokeo yake katika mtihani wa kitaifa. Binti Jitihada anajitoma katika huba na Siti Mlungwi, mjukuu wake Bwana Hasidi. Hasidi mkubwa wa aila ya Jitihada.
Je, Saida ataweza kukabiliana na changamoto hizi na kusimama imara dhidi ya upinzani unaoikumba familia yake?