Zachary Oreri

Zachary Oreri

  • No ratings found yet!

Talanta si Ndumba by Zachary Oreri

KShs700.00
Dunia imekataa kuwatambua watu kulingana na uwezo na juhudi zao maishani. Mara nyingi tunafumba macho tusibaini kwamba kila mwanadamu amejaliwa talanta ambazo hazitegemei jinsia ya mtu ili kunawiri. Katika riwaya hii ya Talanta si Ndumba, mwandishi ameangazia suala la kutambua uwezo wa binadamu pasi kuegemea kigezo cha jinsia. Talanta si Ndumba ni riwaya iliyojaa mseto wa matukio ambayo mengine yanaibua hisia za huruma na majuto. Mwinyi Mshaufu anakumbana na vitendawili vya maisha ambapo anafeli kuvitegua! Anajaliwa na watoto wasichana ambao anawaona kama wasiofaa kisa na maana ni wa kike. Mshaufu anajiona kama mzazi aliyefeli na kuamini kwamba kukosa mtoto wa kiume ni sawa na kuishi bila mrithi wa mali na nafasi alizotunukiwa. Anamfurusha mkewe Siwazuru pamoja na wanawe Mwenge, Lulu na Hariri. Baina ya machozi na rai za wanawe kumwomba baba yao awaonee imani, Mshaufu anashikilia kani kwamba maji kamfika shingoni. Siwazuru pamoja na wanawe wanakaribishwa na Bibi Nyamwange ambaye anawashauri na kuwapa makao.Wanawe Siwazuru wanatia bidii masomoni na hatimaye kufaulu pakubwa. Talanta zao zinabainika wazi, wanavuma na kujulikana kwingi. Habari hizi zinamfikia baba yao ambaye anazipokea kwa majuto makubwa. Licha ya mtengo uliozuka, binti zake Mshaufu wanaamua kumsamehe na kuzika tofauti zao. Kwa kweli, kazi hii imejaa mafunzo ainati ambayo lengo lake kubwa ni kumhamasisha msomaji kwamba haifai kumbagua mtu kwa kuzingatia jinsia yake! Kila mtu, wa kike au kiume, ana uwezo sawa!
delivery

QUICK DELIVERY

Swift dispatch

ONLINE PAYMENT

Multiple options

EXPERT SUPPORT

Help when you need it

WIDE VARIETY

Thousands of books

GLOBAL SHIPPING

Worldwide delivery

Shopping cart
Sign in

No account yet?

Shop
0 Wishlist
0 items Cart
My account