Zachary Oreri

Zachary Oreri

  • No ratings found yet!

Natamani Jana by Zachary Oreri

KShs600.00
Kweli Jana si Leo. Jana tuliishi kama vijana, Leo mambo ni tofauti. Kauli hii imedhihirika wazi kwenye riwaya hii iitwayo Natamani Jana ambapo wahusika mbalimbali wanatadarukiwa na ukweli mchungu kwamba ujana kama moshi, ukienda haurudi. Vijana wanazama kwenye bahari ya maisha, wanashindwa kuhimili tufani za ujanani ambazo zinageuka maafa na kuwameza wengine, huku wengine wakibaki kujuta. Mwanaisha anakiuka mipaka na kwenda kinyume na wosia wa wazazi wake, anatoroka nyumbani na kwenda kutafuta kile anachokiita uhuru wake lakini hatimaye maji yanamfika shingoni. Baadhi ya wahusika akiwemo Zawadi wanajaribu kutumia ujana wao visivyo na hatimaye wanaishia kujiuma vidole. Maisha yanawapa shubiri na kuishia pabaya. Hata hivyo, jambo linalobainika wazi ni kwamba kazi hii bunilizi inafaulu kumsafirisha msomaji katika anga ya kutalii maisha na changamoto zinazowakumba vijana pamwe na wazazi kujaribu kuwadhibiti. Licha ya wengi kushindwa kuhimili vizingiti vya ujanani, wapo wengine wanaofaulu. Natamani Jana ni riwaya iliyo na visa na matukio yaliyosukwa yakasukika.Visa hivyo vinakusudiwa kumsisimua msomaji na kumsafirisha hadi katika ulimwengu wa vijana walio nguzo za jamii. Mwandishi amefaulu kumsawiri mtu yeyote aitwaye kijana kwamba yeye ni mhimili mkubwa katika ujenzi wa jamii. Hivyo basi, ipo haja ya kwenda na wakati.
delivery

QUICK DELIVERY

Swift dispatch

ONLINE PAYMENT

Multiple options

EXPERT SUPPORT

Help when you need it

WIDE VARIETY

Thousands of books

GLOBAL SHIPPING

Worldwide delivery

Shopping cart
Sign in

No account yet?

Shop
0 Wishlist
0 items Cart
My account