QUICK DELIVERY
Swift dispatch
ONLINE PAYMENT
Multiple options
EXPERT SUPPORT
Help when you need it
WIDE VARIETY
Thousands of books
GLOBAL SHIPPING
Worldwide delivery
0794 233 261
KShs800.00 KShs600.00
In stock
Profesa Kithaka wa Mberia anafundisha na kufanya utafiti katika Idara ya Isimu na Lugha, Chuo Kikuu cha Nairobi, Nairobi, Kenya. Mbali na kufundisha na kufanya utafiti, anajishughulisha na uandishi wa mashairi na tamthilia. Tamthilia yake maarufu iitwayo Kifo Kisimani ilikuwa kitabu cha lazima katika mtihani wa kidato cha nne nchini Kenya kuanzia 2006 hadi 2012. Tamthilia yake nyingine iitwayo Natala ilikuwa kitabu cha kutahiniwa katika vyuo vya walimu, pia nchini Kenya, kuanzia 2005 hadi 2016. Mwandishi amewahi kukariri mashairi yake katika maeneo kadhaa ikiwa ni pamoja na Kenya, Tanzania, Iran, Marekani, US Virgin Islands, United Arab Emirates, Upolanzi, Ujerumani na Italia.
Mbali na Doa, Kifo Kisimani na Natala, Profesa Kithaka wa Mberia amechapisha vitabu vingine ambavyo ni Mchezo wa Karata (mashairi), Bara Jingine (mashairi), Redio na Mwezi (mashairi), Msimu wa Tisa (mashairi), Rangi ya Anga (mashairi) na Maua Kwenye Jua la Asubuhi (tamthilia). Diwani nyingine zake mbili za mashairi, Mvumo wa Helikopta na Bustani ya Miungu (huenda vichwa hivi vikabadilkika), zinatarajiwa kuchapishwa mwaka huu na mwaka ujao mtawalia.
Swift dispatch
Multiple options
Help when you need it
Thousands of books
Worldwide delivery
No account yet?
Create an Account
Reviews
Clear filtersThere are no reviews yet.