Jasusi na Mwanadiplomasia nguli Joseph Kaduma ama Joe kama alivyozoeleka kuitwa akishirikiana na wenzake wanafanikiwa kumtoa madarakani Rais Sylvester Costa na hivyo kumweka mmoja wa mwenzao kuwa Rais wa Stanza, Habib Chamchua.
Lakini hali inageuka kuwa tofauti na walivyokusudia, Korea Kaskazini nchi waliyoitumia kuwasaidia kutimiza azma ile ya kumtoa Rais Costa madarakani wanakuja na matakwa mazito yasiyotekelezeka.Joe na Rais Habib wanakuwa katika wakati mgumu wa ama kutekeleza takwa lile ama kuingia uadui na Korea Kaskazini.
Wanaamua kutokutekeleza na hivyo kuingia kwenye msuguano mzito na Korea Kaskazini. Hali inakuwa ya sintofahamu kubwa hadi kupelekea Rais Habib kupotea Ikulu.
Ni mtafutano usio wa kawaida.