QUICK DELIVERY
Swift dispatch
ONLINE PAYMENT
Multiple options
EXPERT SUPPORT
Help when you need it
WIDE VARIETY
Thousands of books
GLOBAL SHIPPING
Worldwide delivery
0794 233 261
KShs1,000.00 KShs800.00
Udhalimu wa wanawake na wanaume ni suala la kawaida. Kazi hii inadhihirisha uhalisia wa maisha katika familia nyingi za kisasa ambapo kuna ufeministi ambapo hata mwanamke anahisi kuwa nguzo ya familia. Maisha hayo ni sawa na yale watu waliyokuwa wakiishi katika nchi dhahania ya Sokoya, iliyokuwa na makabila mawili yaani Wakomoro na Warambi.
Riwaya yenyewe, inadhihirisha dhahiri shahiri jinsi wanaume wanavyodhulumiwa na wake zao. Bw. Mkata ni mfano bora anayedhalilishwa na mkewe Zekelina, mwanamke mashuhuri na maridadi katika mavazi yake kwa sababu ya hali yake ya uchechefu wa pesa. Latifu pia anadharauliwa na mchumba wake Firinda anayetambua kuwa hajatahiriwa kwa mujibu wa utamaduni wa Rambi.
Kinyume na matarajio, mahusiano yanazuka wakati ambapo wanawake wanawapenda wanaume na kuvuka mipaka na kutangaza hisia zao. Peremina anamchumbia Isma naye Firinda anamsalitikia Latifu na mahusiano hayo mawili yanaishia kwenye machozi.
Maoni ya wasomaji…
Anuani “Chachu za waja” inaafiki matukio yaliyoangaziwa kwenye kazi yenyewe. Pengine hakuna anuani bora zaidi ya Chachu za waja kusawiri dhamira ya mwandishi.
Mwandishi ametumia mbinu ya kipekee ya chachu katika harakatio za kuunda kazi yake kuonesha kwamba, swala analolizungumuzia lipo na waathirika ni wengi.
Swift dispatch
Multiple options
Help when you need it
Thousands of books
Worldwide delivery
No account yet?
Create an Account
Reviews
Clear filtersThere are no reviews yet.