Doa la Ndoa na Hadithi Nyingine ni mkusanyiko wa hadithi fupi za kuvutia zilizoandikwa na waandishi
ambao wamedhihirisha ukwasi mkubwa wa lugha ya Kiswahili pamoja na ustadi wa kuumudu utanzu
wenyewe. Hadithi hizi zinawasilisha mitazamo tofauti kuhusu masuala mazito katika jamii kama vile
ajira, mapenzi, ndoa, unafiki, usaliti na tamaa ya mali. Zinaangazia mashaka tipitipi yanayowakumba
vijana wa kiafrika na familia za kisasa, zikibainisha uhalisia wa maisha ya binadamu.
Kitabu hiki kimejumuisha simulizi zilizosheheni taharuki ya kusisimua, uwezo wa kubana matukio,
mwondoko wa haraka, na ucheshi wa aina yake. Ni kazi inayowalenga wapenzi wa fasihi ya Kiswahili
wanaotamani kuzamia masuala muhimu katika maisha ya kila siku kwa mtazamo wa kiafrika .
Reviews
Clear filtersThere are no reviews yet.