Showing all 8 results

USHANGA by Rutere Shenver

KShs550.00
  • Ushanga ni riwaya inayosimulia kuhusu safari ya kusaka ushanga wa adhama kubwa wa kifalme ambao unazua mtafaruku mkubwa na kuchonganisha falme nyingi. Kupotea kwa ushanga huu kunasababisha matatizo si haba.

Doa la Ndoa na Hadithi Nyingine

KShs800.00 KShs700.00
Doa la Ndoa na Hadithi Nyingine ni mkusanyiko wa hadithi fupi za kuvutia zilizoandikwa na waandishi ambao wamedhihirisha ukwasi mkubwa wa lugha ya Kiswahili pamoja na ustadi wa kuumudu utanzu wenyewe. Hadithi hizi zinawasilisha mitazamo tofauti kuhusu masuala mazito katika jamii kama vile ajira, mapenzi, ndoa, unafiki, usaliti na tamaa ya mali. Zinaangazia mashaka tipitipi yanayowakumba vijana wa kiafrika na familia za kisasa, zikibainisha uhalisia wa maisha ya binadamu. Kitabu hiki kimejumuisha simulizi zilizosheheni taharuki ya kusisimua, uwezo wa kubana matukio, mwondoko wa haraka, na ucheshi wa aina yake. Ni kazi inayowalenga wapenzi wa fasihi ya Kiswahili wanaotamani kuzamia masuala muhimu katika maisha ya kila siku kwa mtazamo wa kiafrika.

UDURUSU WA FASIHI SIMULIZI

KShs400.00 KShs350.00
Ni mwongozo mwafaka wa kuelekeza uchambuzi wa Tanzu na vipera mbalimbali vya Fasihi SIMULIZI.

IMARISHA USHAIRI by Rutere Shenver

KShs500.00
Utafiti umedhihirisha kuwa matokeo ya ushairi wa kiswahili miongoni mwa wanafunzi umekuwa ukidorora siku baada ya siku kutokana na madai kuwa ushairi ni utanzu mgumu ulio na istilahi nyingi tatanishi. IMARISHA USHAIRI ni kitabu kinachochanganua ushairi wa kiswahili kwa njia rahisi na ya kuvutia. Kimefafanua ushairi kwa kina na kutoa vielelezo vya kutosha. Isitoshe, kimekusanya msururu wa mitihani ya kitaifa; maswali pamoja na majibu