Title: Nyota ya Kudurusu Sarufi na Matumizi Ya Lugha
Series: Msururu wa Scanner
Author: Toroitich Patrick Yegon
Target Readers: Wanafunzi wa shule ya Upili.
Kitabu hiki kimeandikwa kwa lengo la kuwafunulia walimu, wanafunzi na wapenzi wote wa Kiswahili siri ya kujua sarufi ya Kiswahili, kwani asiyejua sarufi hajui Kiswahili. Maswala haya yameshughulikiwa: Umuhimu wa kusoma sarufi ya Kiswahili, namna ya kutathmini na kujifundisha maswala ya sarufi, changamoto zinazowakumba wanafunzi katika uelewa wa sarufi, stadi za kudurusu sarufi, maswali ya kudurusu viungo vya sarufi, mitihani miigo na ya kitaifa pamoja na majibu kwa maswali yote.