Kinyonga alishangaa kuona upinde wa mvua ukiwa na rangi za kupendeza. Rafiki yake Mwewe, alikubali kumpeleka kwenye upinde, walipokuwa juu alifurahi sana mpaka akapoteza utulivu. Alishindwa kumshikilia Mwewe, akatumbukia kwenye upinde na kuanguka chini.
Kitabu cha Kinyonga kina mafunzo mengi kwa watoto. Aidha kitaboresha usomaji na kumuwezesha msomaji kutambua majina ya baadhi ya wanyama, ndege na wadudu. Pia kinafunza kuhusu rangi za upinde.