Mitego Kisasa na Hadithi Nyingine ni mkusanyiko wa hadithi fupi unaojumuisha jumla ya hadithi kumi na mbili. Visa vinavyojumuishwa humo ndani ni taswira ya jamii ya sasa. Anthologia hii inaangazia watu wa umri mdogo, wastani na hata wale wazee. Mkusanyiko huu ni madhubuti kwa wanafunzi wa sekodari mwandamizi, vyuo na shule zinazofunza lugha ya Kiswahili. Aidha, mpenzi wa fasihi aliyekita mizizi katika tanzu hio, na yule anayetazamia kujifunza Fasihi Andishi kwa jumla atafaidika pakubwa. Kupitia mkusanyiko huu, utagundua maudhui kama vile: unafiki, wizi, dini, mapenzi, ndoa, uchawi na mazingaombwe, uongozi mbaya ,na nafasi ya vijana na kina mama katika jamii.
Mwandishi amezamia katika mbinu za lugha na kuonyesha jinsi jamii imekumbwa na changamoto nyingi na kuna uwezekano wa kuimarika iwapo matatizo hayo yanasuluhishwa. Kupitia tashtiti na mtindo anuwai, mwandishi anakusudia kuwa utaburudika na kupata mafunzo.
Reviews
Clear filtersThere are no reviews yet.