Mwaisambe alipata taarifa kwamba katika jimbo lao la Matusitusi kulikuwako na mganga mashuhuri. Mganga huyo aliwatibu watu kwa dawa za kienyeji alizokuwa nazo daima. Basi baada ya kusikia habari kumhusu mganga huyo, Mwaisambe aliamua kwenda kumtembelea.
Ndugu Mwaisambe anaonekana kuishi maisha ya kubahatisha. Ni mfano wa vijana wanaoonekana kukosa ruwaza, wanabebwa hobelahobela na upepo wa nakama na kuwaangamiza. Mwaisambe yu safarini kumtafuta mganga mashuhuri asiyemjua asili wala fasili yake. Anapanda milima na kuivuka miamba hadi katika eneo la Kivunja Kimya. Atafaulu kumpata mganga wake? Jisomee upate kujua…
*
Bwana Elishaphan Wachira ni miongoni mwa waandishi wanaochipuka kwa kasi sana. Anajikusuru daima kuandika kwa lugha ya Kiswahili na kukiendeleza. Kwa sasa ni mwalimu wa Kiswahili katika shule ya upili ya Wasichana ya Rarakwa katika Gatuzi la Murang’a. Anajaribu kwa udi na uvumba kukiendeleza Kiswahili kupitia kazi bunilizi. Kwa sasa anamiliki shahada ya ualimu kutoka Chuo Kikuu cha Kenyatta.
Reviews
There are no reviews yet.