Tuzo za Usafi ni kitabu cha wanafunzi wa gredi za chini katika shule ya msingi. Kazi bunilizi hii inazingatia mahitaji yote ya mfumo mpya wa elimu (mtalaa wa umilisi) kama vile ujenzi wa masuala mtambuko. Utajiri mkubwa wa yaliyomo ni burudani katika lugha sanifu na msamiati teule ambao umeshiba mafunzo kemkemu ya maadili. Visa sisimuzi vimesukwa ili kumpa mtoto ilhamu ya kutaka kujua zaidi na kumjengea uraibu wa kusoma kwa ufasaha. Usafi wa mwili ni mazoea mazuri. Umuhimu wa usafi ni upi? Utaratibu wa usafi wa mwili ni upi? Vifaa gani hutumika kuusafisha mwili?
Mwandishi wa kitabu hiki, Timothy Omusikoyo Sumba ni mtaalamu wa saikolojia na fasihi ya watoto. Ameandika vitabu chungu nzima ambavyo vimeidhinishwa na Taasisi ya Kukuza Mitaala ya Kenya (KICD) pamwe na Research Triangle International (RTI).
Reviews
Clear filtersThere are no reviews yet.