QUICK DELIVERY
Swift dispatch
ONLINE PAYMENT
Multiple options
EXPERT SUPPORT
Help when you need it
WIDE VARIETY
Thousands of books
GLOBAL SHIPPING
Worldwide delivery
0794 233 261
KShs449.00 KShs399.00
In stock
Kwikwi za vilio vya bi harusi zinasikika kwa mbali. Kalazimishwa kuwa mke wa mtu, ndoto yake imevunjwa na kusagwasagwa bila ya huruma. Kavalishwa gauni la kiyombo, kichwani katundikwa taji la leso lililopachikwa viwangwa vinavyong`aa.
Machozi yanamtoka machoni na kuuharibu wanja aliopakwa. Naam machozi. Si machozi ya furaha bali ya karaha. Binti wa miaka kumi na mitatu hatimaye anaenda kufunga ndoa na mzee wa miaka tisini. Je huu ni mwisho wa ndoto yake Bi harusi aliyoiwekeza toka angali kinda? Ama ndio mwanzo wa shida zake kuisha?
Mwanzo wa Mwisho ni riwaya iliyojikita nchini Fokota. Wanawake wa jamii hii wametengwa na kudharaulika. Wao hawana kauli mbele ya wanaume. Mateso, binti aliyekulia kwenye utandabui wa unyanyapaa alijikusuru kuing`oa mizizi hiyo. Je atakumbana na yepi njiani? Na je atafaulu?
Mwarabu Omari Mwarabu ni mwandishi anayechipuka kwa kasi mno kwenye sanaa ya utunzi wa hadithi za kiswahili. Alizaliwa Bodo, Kaunti ya Kwale mwaka wa 2000. Mwanzo wa Mwisho ni riwaya yake ya pili baada ya ile ya kwanza iitwayo Daraja la Mauti. Kwa sasa ni mwanafunzi wa chuo kikuu cha Rongo , anasomea Shahada ya Takwimu na Tarakilishi. Pia ni mwanachama wa CHAWAKAMA Kenya.
The Guy Who Fired His Boss is a book you must need to read if you are starting a new business or building one. It has helped many entrepreneurs find their space and given others the courage to start. Those who have been in business they have had their motivation renewed and those who feel lost rediscover the direction of their business.
Swift dispatch
Multiple options
Help when you need it
Thousands of books
Worldwide delivery
No account yet?
Create an Account
Reviews
Clear filtersThere are no reviews yet.