Showing all 15 results

Mimi Na Rais (The President and I) by...

KShs1,200.00
Joseph Kaduma, Shushushu na Mwanadiplomasia nguli anaingia katika sintofahamu kubwa kati yake na Rais Sylvester Costa wa Jamhuri ya watu wa Stanza.Joe, kama wengi walivyozoea kumuita serikalini ni muhanga kama walivyo wengi nchini humo kutokana na utawala dhalimu, usiozingatia misingi ya utawala bora na haki, uliojaa rushwa na unyanyasaji wa kila aina chini ya Rais Costa. Katika kuaminiwa kimashaka na Rais Costa, Joe anapewa kazi ya kurudisha mahusiano ya kidiplomasia kati ya Stanza na Korea Kaskazini na akiitumia nafasi hii yeye akiongoza baadhi ya marafiki zake waliopo ndani ya serikali na Idara ya Usalama wa Taifa wanaamua kujaribu kuleta mabadiliko ya kiuongozi nchini Stanza. Rais Sylvester Costa anawashtukia na hapo anaanza kuwawinda Joe na genge lake lote ili alimalize kwa kutaka kuleta usaliti dhidi yake. Joe anaingia kwenye vita kubwa ya kuokoa maisha yake, familia yake, rafiki zake na mali zake dhidi ya mkono wa Rais dhalimu Sylvester Costa. Ni ama yeye ama Rais.

Afuata Mkondo Mbaya

KShs500.00 KShs380.00
Title: Afuata Mkondo Mbaya Author: Toroitich Patrick Yegon Target Class: Teenage Readers From Class 7 Badu, kijana mwenye umri mdogo anaamua kutoroka kuwachia masomo katika darasa la sita na kwenda mjini kutafuta maisha mapya. Afuata Mkondo Mbaya ni hadithi ya Kupendeza iliyojaa sadfa na matukio yenye kutambua ukweli wa kusikitisha. Mwandishi ametumia ploti sahili na kuzungumzia matukio kwa lugha sahili inayofanya hadithi kuvutia Zaidi. Masimulizi yake yanadhihirisha uovu unaondelezwa na vijana, Badu akiwa mfano wa vijana waliopotokwa na nidhamu katika jamii. Hii ni hadithi adhimu.