Jasiri ana Kengeza. Kengeza hilo halimpi amani. Linamsumbua maishani. Hilo kengeza linayaunganisha maisha yake ya zamani na usasa. Kalipata ujanani. Amekataa kulizika katika kaburi la sahau. Je, Jasiri atapata tiba ya kengeza hilo analopenda, kulificha pembeni mwa kijoyo chake? Anagundua pia marehemu babake kaaga dunia kutokana na hilo kengeza. Je, haya makengeza ndiyo nini? Ni masimulizi yanayonata, yaliyosheheni taharuki na maudhui mazito.
Kuhusu mwandishi
Shisia Wasilwa ni mwandishi na mwanahabari stadi wa siku nyingi. Aliwahi kuhudumu na Shirika la Habari nchini Kenya-KBC, China Radio Kimataifa, Citizen Tv na Radio, BBC na Deutsche Welle-DW. Baadhi ya kazi zake ni pamoja Makovu ya Uhai na Dunia Tambara Bovu. Alihariri Ndoto ya Almasi chake Ken Walibora, mwongozo wa Utengano wa Said. A. Mohammed miongoni mwa kazi nyingine teule. Kwa sasa anazamia shahada ya uzamili katika masuala ya mawasiliano katika chuo Kikuu cha Aga Khan.