Showing all 9 results

Mwongozo wa BEMBEA ya Maisha

KShs400.00 KShs350.00
Ni mwongozo wa kumsaidia mwanafunzi kuchambua Tamthilia ya BEMBEA ya Maisha kwa mujibu wa wahusika, sifa za wahusika, fani, dhamira, msuko na maudhui

UDURUSU WA FASIHI SIMULIZI

KShs400.00 KShs350.00
Ni mwongozo mwafaka wa kuelekeza uchambuzi wa Tanzu na vipera mbalimbali vya Fasihi SIMULIZI.

Mwongozo wa MAPAMBAZUKO YA MACHWEO na...

KShs500.00 KShs450.00
Huu ni mwongozo tu. Utamsaidia mwanafunzi katika ufundi wa kuchambua HADITHI fupi za diwani ya MAPAMBAZUKO YA MACHWEO. Inasisitizwa kwamba mwanafunzi asome kwa kina hadithi zote kwanza ndiposa atumie mwongozo huu. Bila hiyo ni kazi bure. Mwongozo ni ramani tu. Msafiri asipofunga safari, hafiki popote.

NITAAMINI NIONAPO

KShs1,000.00 KShs900.00
Wema hukuza mema, mikosi na tufani za maisha zilimnyang'anya Stella wazazi. Akajikutamikonono mwa wenyeji walalahoi. Nap wakamuani. Hatua kwa hatua alipanda ngazi kwa usaidizi wa kijana Ombaomba. Akawa awika ndani na nje ya nchi kupitia talanta yake.

Kivuli Kinaishi

KShs460.00
'Kivuli Kinaishi' ni tamthilia iliyoandikwa kwa kutumia dhana ya Giningi; makazi yaliyo ndani ya vichwa vya watu wa Unguja na Pemba na ambayo yanaogopwa sana na kuhusishwa na vitisho na hadithi kadhaa. Serikali ya Giningi yenye amri moja tu inaongozwa na Bi. Kirembwe akisaidiwa na wazee. Amali kuu ya Giningi imeonyeshwa kuwa ni ukatili na hivyo kanuni kubwa ni kujaribu kuwatoa watu kutoka dunia hii tuijuayo na kuwapeleka katika dunia ya siri, Giningi. Mwandishi amefaulu sana kutumia U-giningi katika kuchora picha fulani tata inayofanana na Giningi. Mhusika Mtolewa anadhihirisha mapambano ya kifikra yanayotokea kati ya wana-Giningi na Bi. Kirembwe na kuonyesha bayana mchezo huu unavyoambatana na ukweli wa maisha, na zaidi jinsi ulivyo mchezo wa wakati.

Sauti ya Dhiki (Toleo Jipya)

KShs440.00
Diwani hii - inayosheheni mashairi kuhusu utamaduni, mapenzi, nasaha, siasa, mambo ya kinyumbani, n.k. - ilitungwa baina ya 1969 na 1972 ambapo mtunzi alikuwa kifungoni baada ya kupatikana na hatia ya kuwachochea watu ili waipindue Serikali ya Kenya kwa kutumia silaha. Kwa hivyo, unapoisoma diwani hii hutaweza kujizuia kuona athari ambayo kifungo huweza kuwa nayo kwa mfungwa. n nJambo la maana sana kuhusu diwani hii ni kwamba mtunzi ameweza kuzungumzia mambo ya kisasa, kama alivyofanya katika shairi la 'Usiniuwe!', bila kupotoka na kutafuta mifano ya kigeni. Hili ndilo lililompa Shihabuddin Chiraghdin, mmoja wa wataalamu mashuhuri wa lugha ya Kiswahili, kusema katika utangulizi wake kwamba, ingawa mtunzi ameingiliwa na athari za kigeni kwa ajili ya elimu aliyoipata shuleni, 'hakukubali kuzongwazongwa na athari hizo, hivyo mashairi yake hayana maingilio ya miundo ya kigeni hata chembe, na mawazo yake yote yameambatana na Uswahili na Uafrika kwa jumla'. n nKitabu hiki kitawafaa wale wapendao kusoma mashairi ya Kiswahili ya kiwango cha juu, na vilevile wanafunzi wa fasihi ya Kiswahili katika shule za sekondari na vyuo vikuu.

Mfalme Edipode

KShs460.00
Mchezo huu ni tafsiri ya mmojawapo wa michezo ya misiba iliyo mashuhuri iliyotungwa na yule mwandishi wa Kigiriki, Sofokile, kiasi cha miaka 420 kabla ya Kristo. Unatuwekea mbele yetu hadithi nzuri mno ya mfalme ambaye, pamoja na kuwa na moyo laini, ana ndweo ya kiburi cha kuzawa nacho. Kiburi hicho ndicho kinachompeleka kwenye kifo kiovu baada ya kumuua babake na kumuoa mamake bila ya kujua. n nKatika tafsiri hii iliyofanywa kutokana na nakala kadha wa kadha za Kiingereza, Samuel Mushi ameuhifadhi ule moyo na tabia ya ushairi asilia wa Kigiriki na papo hapo akashikamana na mwendo wa ushairi wa Kiswahili kwa kadri inavyowezekana. Katika utangulizi wake anakokoteza kwamba ingawa mchezo huu ulitungwa kwa mujibu wa utamaduni wa Kigiriki wa kale, wahusika wake na hisia zao ni za kiulimwengu mzima na, kwa hivyo, mchezo wenyewe unaweza kuchezwa katika mazingira ya Kiafrika.

Kwenye Ukingo wa Thim

KShs375.00
Tamthilia ya Kwenye Ukingo wa Thim inaonyesha migogoro iliyopo baina ya mahitaji ya mila na mahitaji ya maisha ya kisasa. Mwandishi amefaulu kuonyesha mvutano huo unavyoweza kutokea na athari zake kwa wanaohusika.

Mashetani

KShs440.00
Kitaru na Juma ni vijana wawili ambao wanasoma katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, waniotoka katika familia mbili za kikabaila ambazo zenye historia zilizofanana na zilizotofautiana.Ukabaila wa familia ya Juma ni 'ubwanyenye', na ukabaila wa familia ya Kitaru ni 'unaizi'.Katika mchezo huu ukabaila wa aina ya familia ya Juma umeanza kung'olewa, lakini ukabaila wa aina ya familia ya Kitaru ndiyo kwanza unatiliwa mbolea na uzalendo. Daina ya Kitaru na Juma kuna mapenzi na chuki, shaka na wasiwasi, tuhuma na dhambi, huku wakitafuta uhusiano wa maana katika wakati na hali waliyonayo.