'Kiswahili Dadisi' ni msururu wa vitabu vilivyoandikwa kwa utaalamu na upekee ili kufanikisha ufundishaji na ujifunzaji wa mahitaji ya Mtaala wa Umilisi. Vitabu hivi vitawawezesha wanafunzi kupata ufahamu wa lugha kupitia stadi za Kusikiliza, Kuzungumza, Kusoma na Kuandika, na vilevile Sarufi, kupitia mazoezi murua ambayo pia yanakuza umilisi uliopendekezwa, maadili na kufahamisha kuhusu masuala mtambuko. Katika
'Kiswahili Dadisi', Kitabu cha Mwanafunzi, Gredi ya1 utapata:
n
n - Mada zilizopangwa kwa kuzingatia muainisho wa mtaala.
n - Mifano halisi ya matumizi ya lugha kimuktadha.
n - Mazoezi ya kuchangamsha na kufikirisha ambayo yanawashirikisha wanafunzi moja kwa moja.
n - Vifungu vya kuburudisha na vinavyoendeleza ujifunzaji.
n - Nyimbo za kusisimua ambazo zitawachangamsha na kuwaburudisha wanafunzi.
n - Picha za rangi, zenye mvuto wa kipekee na ambazo zinachangia pakubwa katika ujifunzaji wa mwanafunzi.
n - Mazoezi ya kuwahamasisha wanafunzi kuendeleza ujifunzaji nje ya darasa.
n - Mazoezi ambayo yatawashirikisha mwanafunzi kutumia vifaa vya kidijitali katika ujifunzaji.
n - Jinsi ya kumshirikisha mzazi au mlezi kuimarisha ujifunzaji.
n
n
'Kiswahili Dadisi', Kitabu cha Mwanafunzi Gredi ya 2 kina Mwongozo wa Mwalimu ambao pia una mazoezi na maelekezo tosha ambayo mwalimu anahitaji ili kumwongoza mwanafunzi aweze kufaulu katika somo la Kiswahili.