'Maneno ya Mwanzo' ni kitabu kinachonuiwa kujenga msingi thabiti wa kusoma. Kitabu hiki kimekusudiwa wanafunzi waliomaliza shule za chekechea na kuanza masomo yao katika shule za msingi. Kitabu hiki kinafaa kutumiwa na wanafunzi wa darasa la kwanza.
n
nSifa kuu za kitabu hiki ni kama zifuatazo:
n
n - Utambuzi wa herufi kuu za alfabeti ya Kiswahili.
n - Utambuzi wa maneno, hasa nomino na vitenzi.
n - Uhusishaji wa herufi kuu za alfabeti ya Kiswahili na neno pamoja na tungo.
nKuzua uzoefu wa kutamka na kusoma herufi, maneno na sentensi za Kiswahili.
n - Uteuzi bora wa msamiati uliokadiriwa kwa mujibu wa kiwango cha darasa hili.
n - Kurahisisha ufahamu wa maneno kupitia picha zenye rangi za kuvutia na zenye kusisimua.
n - Kusoma sentensi sahali zenye miundo myepesi kulingana na matakwa ya silabasi.
n - Kujua maumbo ya herufi na namna maneno yanavyoandikwa kwa njia ya mistari.
n
nFauka ya yote haya, kumtangulizia mwanafunzi aliyemaliza shule ya chekechea na kujiunga na darasa la kwanza, kuanza kusoma vitabu vya kiada na ziada kwa njia nyepesi. Bila shaka, huu ni mwanzo wa kusoma kupitia ngazi tatu: kwa njia ya alfabeti, maneno na sentensi.
n
n
'Maneno ya Mwanzo' ni kitabu kinachofaa kutumiwa pamoja na kitabu cha Kiswahili Sanifu, Darasa la Kwanza na la pili. udongo upatilize ungali maji.