Showing 941–960 of 20714 results

Maskini Milionea

KShs540.00
'Maskini Milionea na Hadithi Nyingine' ni mkusanyiko wa hadithi fupi zinazoakisi hali katika maisha ya wanadamu; hisia zao, changamoto na ufanisi wao. Ubora wa hadithi katika mkusanyiko huu haumo tu katika uanuwai wa fani na maudhui, bali pia kwenye mseto wa ufundi wa wachangiaji ambao wana asili na mitazamo tofautitofauti. n nHadithi hizi zilizoandikwa na waandishi kutoka maeneo mbalimbali ya Afrika Mashariki ni mchango mkubwa katika utanzu wa hadithi fupi za Kiswahili.

Waja Leo

KShs440.00
'Waja leo' ni mkusanyiko wa mashairi ya aina yake yanayomulikia kurunzi vipengele anuwai vya waja (binadamu) wa leo. Watunzi wa mashairi katika diwani hii wana tajiriba na falsafa tofautitofauti zinazodhihirishwa na mitindo na maudhui yao mbalimbali. Mashairi yenyewe yameandikwa kwa lugha rahisi kusomeka na kueleweka, yaliyo na mvuto wa ajabu na ambayo yatawafaa wapenzi na wasomi wa mashairi ndani na nje ya mipaka ya asasi za elimu. n nKatika diwani hii, mna utangulizi kwa msomaji wenye maelezo mwafaka kuhusu mbinu ya kuyasoma na kuyachambua mashairi kwa faida ya wasomaji katika shule za upili. Aidha, kuna maswali ya mazoezi kwenye kurasa za mwisho.

Zawadi ya Thamani

KShs365.00
Je, hatima ya maisha ya Nadia ni ipi? Ni zawadi gani ya thamani itakayomwokoa? Je, ni kujiamini kwake au ni ubunifu wake? Je, ni huruma au hisani yake? Je, ni shajara yake inayosema yale ambayo moyo wake unachelea kuyasema? Au labda ni Mwalimu Daniela ambaye amefanikiwa kukitegua kitendawili cha maisha yake? n n'Zawadi ya Thamani' ni hadithi ambayo imesimuliwa kwa lugha nyepesi yenye ubunifu na mvuto mkuu. Upekee wa hadithi hii umo katika uwezo wayo wa kumteka msomaji kuanzia mwanzo hadi mwisho, na wakati uo huo kumpa mafunzo anuwai kuhusu namna ya kukabiliana na changamoto za maisha. Hadithi hii imeangazia masuala mtambuko mbalimbali na kusawiri maadili yanayopendekezwa katika Mtaala wa Daraja ya Awali ya Shule za Sekondari.

Tubadilishe Jina

KShs525.00
Kinyume na sifa na siha yake, kaunti aliyoitawala ilikuwa nyeusi; weusi uliowatia wakazi huzuni kutokana na ulafi na mapuuza ya viongozi. Baya zaidi, sauti za wapinzani dhidi ya umaskini, ukosefu wa ajira na magonjwa zilizimwa. 'Tubadilishe Jina' ni riwaya inayomulika maovu mbalimbali katika jamii yetu ya leo, na madhara yanayotokana na uongozi mbaya. Hadithi hii, vilevile, inaangazia nafasi ya uanaharakati katika kuupiga msasa uongozi ili kudumisha maadili katika jamii.

Mbona Hivi?

KShs510.00
Ni vipi mtoto mdogo kama Sandra anafahamu maneno kama hayo? Tena maneno ambayo si ya Kiswahili, si ya Kiingereza, si ya lugha za kigeni au za kiasili. Yanatoka wapi? Ni nani waasisi wake? Mzee Jarida alijiuliza baada ya kumsikia mjukuu wake akizungumza. Maswali hayo yalipita akilini mwake haraka na kukaribisha fikra nyingi. n n'Mbona Hivi?' ni riwaya ambayo imeandikwa kwa lugha yenye mvuto na upekee. Inaangazia masuala yanayoathiri vijana na kuibua mjadala – mjadala wa kujadiliwa leo, kesho na hata siku za usoni – kuhusu mustakabali wa lugha ya Kiswahili katika jamii.

Wema Waliobaki

KShs570.00
Mazungumzo yao yalikuwa mafupi. Alihitajika nyumbani haraka. Kulikuwa na dharura. Je, nini kilichokuwa kimetokea cha kuibua dharura hii? Ni kipi cha dharura ambacho hakingeweza kupitishwa kwa simu? Si simu zenyewe zinafaa kupitisha jumbe za dharura? n n'Wema Waliobaki' ni riwaya inayoakisi sura mbalimbali za maovu yanayotekelezwa na watu wenye tamaa ya kuvuna wasichokipanda katika jamii ya leo. Ni hadithi inayowasawiri wanaja mii kama nduli wala watu; mamba wanaosubiri kwenye kingo za mito kuwavamia watekamaji wasiokuwa na habari. Hata hivyo, katika jamii iliyogubikwa na giza la ukosefu wa maadili hapakosi mwanga; mwanga unaotokana na wema waliobaki, hata kama ni wachache.

Kitumbua Kimeingia Mchanga

KShs425.00
'Kitumbua Kimeingia Mchanga' ni tamthilia inayozusha mawazo kuhusu tofauti zilizoko baina ya mila na tamaduni za kale na za kisasa kuhusu suala la ndoa. Pia imeshughulikia uhuru wa vijana wa kileo kinyume na matakwa ya wazee wao. Fikirini hakubali kuchaguliwa mke na babake, Bw Mambo na nyanyake, Bi Hoja. Wazee wake wanaona jambo la kumchagulia mtoto wao mke ni jukumu lao. Vilevile, wanamtuhumu Hidaya, msichana ambaye Fikirini anataka kumuoa, kuwa ni kiruka njia, mhuni na muovu. Je, Fikirini atashinda kuwatoa shaka na kuwashawishi wazee wake wamkubalie analolipenda? Je, ndoa ya Fikirini itafanikiwa?

Kiti cha Moyoni na Hadithi Nyingine

KShs590.00
Huu ni mkusanyiko wa hadithi fupi ishirini ambazo zina utamu kutokana na mtindo wa fantasia na mkengeuko wa ukweli kama tunavyoujua wa kila siku.

Heri Subira

KShs510.00
Sabra alihisi kwamba alikuwa ameuvuta uvumilivu wake ukafika mwisho. Alistahimili vya kutosha lakini ikawa nhali ya 'likikatwa kono linamea guu'. Je, mtu huhitajika kusubiri kiasi gani ili apate heri?

Ni Rangi Tu

KShs415.00
Majaaliwa alipokutana na binadamu wenzake alitamani kujichimbia ardhini ajifiche. Waliicheka rangi yake 'iliyochujuka', kama walivyosema wenyewe. Walimhepa na kumkimbia kama mgonjwa wa ukoma! Wakati mwingine Majaaliwa alijutia majaaliwa aliyopewa, lakini alijijasiri akakabiliana nayo kiume. Aliyakabili kama vile simba jike mwenye hasira anavyomkabili adui, na hatimaye! Hatimaye ... n n'Ni Rangi Tu' ni hadithi ya kusisismua iliyoandikwa kwa lugha sahili. Lugha ambayo inateka makini ya msomaji na kumfanya kutaka kuisoma mfululizo bila kukoma. nAlly Mtenzi, mwandishi wa hadithi hii ni naibu wa Mhariri Mkuu katika runinga ya K24, Shirika la Usambazaji habari la Media Max.

Hatima Ya Kubuni

KShs415.00
Wanasayansi, wanaramani mabingwa wameshindwa kutambua kilipokuwa kijiji cha Kubuni na kukiweka juu ya uso wa dunia. Kile wanachojua ni kuwa kijiji chenyewe kilikuwepo, ila sasa hakijulikani kitovu chake. Mzee Pepo tu ndiye aliyeshuhudia kijiji kikitokomea. Anaelezea masaibu yaliyokikumba kijiji hiki kwa namna itakayokuacha wewe msomaji ukistaajabu ... n nMwandishi, Hamad Simai, ni mwandishi mtajika wa riwaya na kazi nyingine za kubuni. Aidha, ni mtaalamu wa teknolojia nchini Zanzibar.

Kivuli Cha Ndoto

KShs340.00
Waama leo ... leo ninaona miale ya mapambazuko ikinijia taratibu ...” Matamanio ya ufanifu ndiyo huwa ndoto inayomwongoza na kumwandisi mwanadamu maishani. Kezi Pasuamende, anaambikwa ubakaji na hatimaye kuhukumiwa kifungo cha miaka 27. Anakosa kusoma hadi chuo kikuu ili aweze kuwa rubani. Je, ataweza kufanikisha ndoto yake ama atalazimika kukubali chochote ilimuradi aweze kuendesha maisha yake? n n'Kivuli cha Ndoto' ni hadithi iliyoandikwa kwa mkono wenye ukwasi wa lugha na uwazi wa kimasimulizi. Ni hadithi ambayo haiishi hamu ya kusomwa tena na tena kwa sababu ya mvuto wake.

Kipendacho Roho

KShs350.00
Bado tulisubiri 'wakaishi raha mustarehe'. Siku hiyo nyanya hakumaliza hivyo… Kadzo anajikuta katika mtego wa hadaa. Alipenda kwa roho, kumbe kipendacho roho.

Mashaka

KShs340.00
Nini ambacho Kiburi hakubarikiwa nacho; mali, ulimbwende au umaarufu? Lakini, vyote hivi havikutosha kumpa raha aliyoisaka maishani. Kwa upande mwingine, Mashaka anakumbana na mashaka kwa sababu ya kiburi cha Kiburi. Sio kwamba Kiburi hakumpenda Mashaka. La, hasha! Alimpenda sana na alikuwa tayari kumwaga mali yake yote, mradi tu ampate. Basi, binadamu huhitaji nini ili kufurahia ukamilifu wa maisha? Hili ndilo swali ambalo mwandishi anauliza katika kisa hiki cha kuburudisha na kuelimisha.

Si Kitu

KShs415.00
Hii ni novela inayoteka nadhari ya msomaji kwa msuko wake wa kipekee. Kupitia riwaya hii, mwandishi anahimiza umuhimu wa kusamehe. Anawakejeli wanajamii wanaoendeleza chuki, kinyongo, kisasi, choyo na usiri - ingawa anasema zipo siri zinazowekwa ili kumlinda mtu.

Mlemavu? Si mimi

KShs365.00
Godfrey Ipalei, kama mhusika mkuu, anajiandikia tawasifu yake kuwatangazia walimwengu kuwa mtu yeyote anaweza kuyafikia malengo yake na kutimiza ndoto zake maishani licha ya changamoto za kimaumbile. Anasisitiza kuwa ulemavu ni wa fikira na mielekeo hasi. Msomaji anatiwa moyo kutambua na kurutubisha kipawa alichonacho.

Ningekuwa na Uwezo

KShs475.00
Je, ungekuwa na uwezo wa kubadili ulimwengu unamoishi, ungeubadili? Ungebadili nini?

Kosa si Kosa?

KShs450.00
Lullu Katanga, mwanafunzi wa uanasheria, anajikuta korokoroni. Akipatikana na hatia, atahukumiwa kifungo bila dhamana. Shahidi wa pekee anayeweza kumsaidia ni mshiriki ambaye ana hatia zake. Je, shahidi huyu atakubali kumsaidia bila mwenyewe kuonekana mkosa?

Upande Mwingine

KShs365.00
Kimako anarejea Kenya baada ya kuishi uhamishoni. Je, ataukabili ulimwengu wa utoto wake uliogeuka au atarudi uhamishoni kusikomweka?

Amri ya Wakati

KShs365.00
Kiu ya Matonga inamsukuma kutaka kuhama kwenda nchi za ng'ambo anakodhani atapata riziki. Lakini vyote ving'aavyo si dhahabu.