Showing 1–20 of 45 results

Mama Kunguru Na Nyoka Mlafi

KShs380.00 KShs350.00
Mama Kunguru na Nyoka Mlafi Author: Badi K. Likokola - Virtue Book Publishers CBC 4-8 Years "Mama Kunguru na Nyoka Mlafi" ni hadithi ya kusisimua kuhusu mama Kunguru na watoto wake. Nyoka, akiwa na tamaa, alipanga kuwadhuru watoto wa Kunguru alipoondoka. Mama Kunguru alirudi, akashangaa na haraka alikimbilia kwa wenzake kwa msaada. Kwa umoja, walimshinda Nyoka. Hadithi hii inatufundisha kuwa umoja ni nguvu na uroho huleta madhara.

Kisa Cha Mvuvi Na Pweza

KShs380.00 KShs350.00
Kisa Cha Mvuvi Na Pweza Justin Mwaniki - Virtue Book Publishers CBC - 6-10 Years Hadithi hii inasimulia mvuvi anayekutana na changamoto nyingi baharini katika jitihada zake za kuvua samaki. Anamkamata pweza, lakini pweza, kwa kushirikiana na wenzake, wanatumia mbinu za kipekee kujinasua mikononi mwa mvuvi. Hadithi hii inafundisha watoto kuhusu umoja, ushirikiano, na kutumia akili kutatua matatizo. Ni hadithi ya kufurahisha na kielimisha.

Mawazo Yamuua Tembo

KShs380.00 KShs350.00
Mawazo Yamuua Tembo Author : Idd Mwimbe - Virtue Book Publishers 5-10 years - CBC Mawazo Yamuua Tembo" ni hadithi ya kusisimua kuhusu tembo aliyejivunia nguvu zake na kuburi dhidi ya wanyama wadogo msituni. Aliwadhihaki wanyama, akiwemo kanga, ambaye alionya tembo kuhusu matendo yake mabaya. Tembo alicheka na kudharau onyo hilo, akijivunia nguvu na uwezo wake. Lakini kadri siku zilivyokwenda, tembo alijikuta akiona shida, na mawazo mabaya yakamwingia, akajikuta akifadhaika zaidi. Nini kilichotokea baadaye? Hadithi hii inatufundisha kuhusu madhara ya kuburi na umuhimu wa unyenyekevu.

WOSIA WA ALI NA HADITHI NYINGINE

KShs900.00 KShs800.00
  1. Hii ni diwani ya HADITHI kumi na tatu za kusisimua. Kila HADITHI imejadili maswala. mbalimbali lakini kwa lugha rahisi inayoeleweka haraka na kutumbuiza. Kila HADITHI ichambuliwe kivyake

SUMU YA PANYA by Isaac Wambedha

KShs1,000.00 KShs900.00
Riwaya hii inasimulia vituko vya Biandis katika Jimbo la Aboke, aliyedai kuwa ni walii wa Mungu. Hulka zake lakini zilikiuka kaida za uwalii wa Mungu. Wazee wakabaki kuduwaa.

ABCh Herufi za Kiswahili by Nasra Oma...

KShs1,000.00 KShs780.00

A Swahili alphabet book suitable for native Swahili-speaking toddlers who are beginning to learn the alphabet and children of all ages who are learning Swahili.

Kitabu hiki kinawafahamisha watoto herufi na maneno ya Kiswahili. Kinawafaa watoto wachanga waliolelewa wakizungumza Kiswahili kujifunza herufi na watoto wa rika zote wanaoanza kujifunza Kiswahili.

Fahari Ya Kuwa Mwafrika by Chiro Martin

KShs1,000.00 KShs860.00
Katika kitabu hiki kwanza tutamuona Kuvuna ambaye ni mtoto wa kike na ameishi kumpenda na kuiga mfano wa mwanamazingira Wangari Maathai. Kuvuna anawaongoza wanafunzi wenzake katika juhudi za kupanda miti shuleni na kupigana na mabadiliko ya anga. Sehemu ya pili tutapatana na marafiki wawili ambao ni Omollo na Wanjiru. Marafiki hao licha ya kua jinsia tofauti, pia wanatoka katika tamaduni tofauti za Kiafrika. Cha kupendeza zaidi ni kua wawili hawa hawatatengana bali watafunzana tamaduni hizo na mwishowe kushawishi shule yao kuandaa tamasha la kitamaduni. Baadaye tutapatana na Amani amabaye anasaidia kikundi hiki kuvumbua historia ya kitajiri ya mwafrika, iliyofichwa na miaka mingi ya ukoloni. Amani kwa usaidizi wa mwalimu wake wa historia anaanzisha kilabu cha historia shuleni. Mwishowe tutapatana na Kiprop ambae ni mpenzi wa teknolojia na uvumbuzi. Anashawishiwa na historia ya uvumbuzi Afrika naye pia anaanzisha uvumbuzi wake ambao tutaona kuwa na msaada mkubwa kwa shule yao na jamii pana.

Nipo Nyumbani by Bellz Wachira –...

KShs850.00
(KISWAHILI VERSION OF: “I AM HOME” ) I Am Home is an emotive poem for children that are going through a parent’s separation or divorce dynamic or just a blended family . The poetry covers real life emotions of a child as they try to make sense of sensitive topics around their difference experiences at home. No matter what happens in the event of separation,a parent who is away, I pray this book evokes the confidence that the child is loved, cherished and seen, at HOME.

Chura na Kipepeo By Mercy Kihugi

KShs500.00 KShs400.00
Chura na Kipepeo is just the beginning of books that bring stories to life in TWO languages, Kiswahili and English! Get ready therefore for a story that's doppelt (German for "double") the fun and a safari of words as we explore languages together.

KISASI BARIDI by Rutere Shenver

KShs1,000.00 KShs800.00
KISASI BARIDI ni riwaya ambayo baadhi ya wahusika wake wanasaka kisasi kwa kuti na mauti. Wana hamu ya kulipiza kisasi kikiwa kingali moto kisije kikapoa na kuwa baridi.

IMARISHA SARUFI by Rutere Shenver

KShs550.00
  1. IMARISHA SARUFI ni kitabu kinachoangazia mada zote za sarufi ya kiswahili katika shule za upili kwa njia rahisi na ya kuvutia. Stadi zote za utunzi wa sarufi katika karatasi ya pili (102/2) zimesawiriwa Kwa undani. Zifuatazo ni sifa zinazokipa kitabu hiki upekee wa hali ya juu: 1. Kimeangazia vipengele vyote vya utahini wa karatasi ya pili kwa njia rahisi. 2. Kina michezo ya visanduku inayowatia wanafunzi ari ya kusoma huku wakicheza. 3. Kina kamusi ya misamiati ibuka pamoja na tafsiri zake kwa kingereza. 4. Kina mazoezi mengi baada ya kila mada ndogo. Aidha, kina mitihani ya vielelezo pamoja na miongozo ya kusahihisha.

IMARISHA USHAIRI by Rutere Shenver

KShs500.00
Utafiti umedhihirisha kuwa matokeo ya ushairi wa kiswahili miongoni mwa wanafunzi umekuwa ukidorora siku baada ya siku kutokana na madai kuwa ushairi ni utanzu mgumu ulio na istilahi nyingi tatanishi. IMARISHA USHAIRI ni kitabu kinachochanganua ushairi wa kiswahili kwa njia rahisi na ya kuvutia. Kimefafanua ushairi kwa kina na kutoa vielelezo vya kutosha. Isitoshe, kimekusanya msururu wa mitihani ya kitaifa; maswali pamoja na majibu

Ngiri Mganga by Emmanuel kariuki

KShs400.00 KShs250.00
This animal story for children looks at the different ways that animals feed in the Savanna. During the wildebeests migration, eating is hard work for some but a picnic for others. It is full of useful lessons in a humorous style.

Kinyonga by Binti Omar

KShs350.00 KShs300.00
Kinyonga alishangaa kuona upinde wa mvua ukiwa na rangi za kupendeza. Rafiki yake Mwewe, alikubali kumpeleka kwenye upinde, walipokuwa juu alifurahi sana mpaka akapoteza utulivu. Alishindwa kumshikilia Mwewe, akatumbukia kwenye upinde na kuanguka chini. Kitabu cha Kinyonga kina mafunzo mengi kwa watoto. Aidha kitaboresha usomaji na kumuwezesha msomaji kutambua majina ya baadhi ya wanyama, ndege na wadudu. Pia kinafunza kuhusu rangi za upinde.

The Real You by Angela Murenga (Swahi...

KShs1,300.00 KShs1,000.00
The Real You (Swahili Version) ni kitabu cha kufungua macho ambachi kinalenga kukuonyesha jinsi ya kufungamana na Mungu aliyeekuumba uwe na kusudi lake kwa maisha yako.

Learning Kiswahili Book by Wambui Kam...

KShs1,200.00 KShs1,000.00
This book is written for everyone, whether you're new to Swahili or already familiar with it. It's written in a clear and straightforward style, perfect for beginners. Whether you are planning to travel to a Swahili-speaking region, work with Swahili speakers, or simply have a love for languages, this book will guide you on your journey to mastering the language.

Mwana Mdogo Wa Mfalme / Le Petit Prin...

KShs1,790.00 KShs1,390.00
First Published in 1943, Le Petit Prince (The Little Prince) is a widely collected book and has been published in 190 languages. This is the only Swahili translation in the world and includes the original drawings by the author, Antoine de Saint-Exupéry. Swahili is the widest spoken African language with more than 300 million speakers worldwide. This is a valuable collector's item and a memorable gift to those who love Le Petit Prince.

Adhabu ya maisha by Elishaphan Wachir...

KShs500.00 KShs450.00
Mwaisambe anamtafuta mganga mashuhuri katika ulimwengu wake mgumu. Je, atampata? Soma upate kujua

Baragumu la Sarufi na ufahamu na ufup...

KShs800.00 KShs760.00
Baragumu ni kitabu cha marudio cha Kiswahili kwa wanafunzi wa shule za upili. Kina maswali ya kcse ya sarufi, ufahamu na ufupisho ya miaka iliyotangulia pamoja na majibu yake