Showing 921–940 of 20714 results

Upeo wa Sarufi kwa Shule za Upili

KShs825.00
'Upeo wa Sarufi' ni kitabu kilichoandikwa kwa utaalamu kikimlenga mwanafunzi wa lugha ya Kiswahili. Kitabu hiki kinaweza kutumiwa na mwanafunzi wa sekondari au wa chuo kama kitabu cha kiada au cha marejeleo. n nUpekee wa kitabu hiki ni kwamba: n
    n
  • Maelezo ya kina yametolewa kwa lugha sahili inayomwezesha mwanafunzi kuelewa vipengele vyote vya sarufi, hata bila ya usaidizi wa mwalimu.
  • n
  • Matumizi ya lugha katika muktadha yanatiwa mkazo kuliko ukariri wa kanuni za sarufi.
  • n
  • Mifano ya matumizi katika sentensi imetolewa kwa kila mada.
  • n
  • Sehemu tata katika sarufi zimefafanuliwa.
  • n
  • Kina mazoezi zaidi ya 200 na majibu yake.
  • n
  • Kinatumia michoro na picha kurahisisha uelewa.
  • n
  • Kinashughulikia silabasi nzima ya sarufi kwa sekondari, kama ilivyopendekezwa.
  • n
nKitabu hiki kimeandikwa na wataalamu wa lugha walio na ukwasi wa tajriba ya uandishi na ufunzaji wa sarufi ya Kiswahili.

Spot On Oral Skills

KShs760.00
Students in secondary schools are required to acquire communicative competence in the English language. They will find this competence useful even after completing school. The Spot On series is designed to equip students with long-lasting English skills. n n'Spot On Oral Skills' provides students and teachers with a resource that explores listening and speaking. It covers oral skills (including speech and intonation), note-taking and oral literature among other areas. n nIt provides: n
    n
  • Information on how to approach and improve oral communication.
  • n
  • Practical activities through which students can practise oral skills.
  • n
  • A variety of exercises and examination-type questions.
  • n
  • Guidelines and answers to the activities and exercises.
  • n
nThe authors are communication experts who have wide experience in the teaching and examination of English language skills.

Spot On Writing Skills

KShs600.00
Students in secondary schools are required to acquire communicative competence in the English language. They will find this competence useful even after completing school. The Spot On series is designed to equip students with long-lasting English language skills. 'Spot On Writing Skills' provides students and teachers with a resource that explores effective writing. n nIt includes: n
    n
  • Mechanics of writing which comprise handwriting skills, spelling and punctuation.
  • n
  • Tips on how to construct a good paragraph right from the word to the sentence and paragraph levels.
  • n
  • The characteristics of a good essay.
  • n
  • An extensive variety of writing exercises.
  • n
  • Sample written texts that are as hilarious as they are informative.
  • n

Spot On Comprehension Skills for Seco...

KShs775.00
Students in secondary schools are required to acquire communicative competence in the English language. They will find this competence useful even after completing school. The Spot On series is designed to equip students with long-lasting English skills. Spot On Comprehension Skills provides students and teachers with a resource that explores reading and comprehension. n n'Spot On Comprehension Skills' has the following distinctive features: n
    n
  • A section on how to approach different types of passages that students are likely to encounter in comprehension exercises.
  • n
  • Information on the reading skills that the students are expected to acquire.
  • n
  • A wide variety of exercises to assist students in acquiring the necessary skills.
  • n
  • Answers to all the questions in the exercises. nThe authors are English language experts who have experience in the teaching and examination of English language skills.
  • n

Spot On Grammar for Secondary Schools

KShs810.00
Students in secondary schools are required to acquire communicative competence in the English language. They will find this competence useful even after completing school. The Spot On series is designed to equip students with long-lasting English skills. Spot On Grammar provides students and teachers of English with a detailed and all-encompassing resource to cater for their grammar needs. It is a reference and practice book for students in secondary schools and colleges. n n'Spot On Grammar' provides: n
    n
  • Straightforward explanation of aspects of English grammar interspersed with practical everyday examples.
  • n
  • Over 200 exercises for practice and also for testing understanding.
  • n
  • Answers to all the questions in the exercises.
  • n
  • Usage tips which pinpoint and iron out confusing aspects of grammar.
  • n
  • Thorough coverage of the grammar content recommended in the English syllabuses in the region. nThis book is meticulously written by English language experts who have a wealth of experience in teaching, and in writing English language books.
  • n

Kivuli Kinaishi

KShs460.00
'Kivuli Kinaishi' ni tamthilia iliyoandikwa kwa kutumia dhana ya Giningi; makazi yaliyo ndani ya vichwa vya watu wa Unguja na Pemba na ambayo yanaogopwa sana na kuhusishwa na vitisho na hadithi kadhaa. Serikali ya Giningi yenye amri moja tu inaongozwa na Bi. Kirembwe akisaidiwa na wazee. Amali kuu ya Giningi imeonyeshwa kuwa ni ukatili na hivyo kanuni kubwa ni kujaribu kuwatoa watu kutoka dunia hii tuijuayo na kuwapeleka katika dunia ya siri, Giningi. Mwandishi amefaulu sana kutumia U-giningi katika kuchora picha fulani tata inayofanana na Giningi. Mhusika Mtolewa anadhihirisha mapambano ya kifikra yanayotokea kati ya wana-Giningi na Bi. Kirembwe na kuonyesha bayana mchezo huu unavyoambatana na ukweli wa maisha, na zaidi jinsi ulivyo mchezo wa wakati.

Sauti ya Dhiki (Toleo Jipya)

KShs440.00
Diwani hii - inayosheheni mashairi kuhusu utamaduni, mapenzi, nasaha, siasa, mambo ya kinyumbani, n.k. - ilitungwa baina ya 1969 na 1972 ambapo mtunzi alikuwa kifungoni baada ya kupatikana na hatia ya kuwachochea watu ili waipindue Serikali ya Kenya kwa kutumia silaha. Kwa hivyo, unapoisoma diwani hii hutaweza kujizuia kuona athari ambayo kifungo huweza kuwa nayo kwa mfungwa. n nJambo la maana sana kuhusu diwani hii ni kwamba mtunzi ameweza kuzungumzia mambo ya kisasa, kama alivyofanya katika shairi la 'Usiniuwe!', bila kupotoka na kutafuta mifano ya kigeni. Hili ndilo lililompa Shihabuddin Chiraghdin, mmoja wa wataalamu mashuhuri wa lugha ya Kiswahili, kusema katika utangulizi wake kwamba, ingawa mtunzi ameingiliwa na athari za kigeni kwa ajili ya elimu aliyoipata shuleni, 'hakukubali kuzongwazongwa na athari hizo, hivyo mashairi yake hayana maingilio ya miundo ya kigeni hata chembe, na mawazo yake yote yameambatana na Uswahili na Uafrika kwa jumla'. n nKitabu hiki kitawafaa wale wapendao kusoma mashairi ya Kiswahili ya kiwango cha juu, na vilevile wanafunzi wa fasihi ya Kiswahili katika shule za sekondari na vyuo vikuu.

Mfalme Edipode

KShs460.00
Mchezo huu ni tafsiri ya mmojawapo wa michezo ya misiba iliyo mashuhuri iliyotungwa na yule mwandishi wa Kigiriki, Sofokile, kiasi cha miaka 420 kabla ya Kristo. Unatuwekea mbele yetu hadithi nzuri mno ya mfalme ambaye, pamoja na kuwa na moyo laini, ana ndweo ya kiburi cha kuzawa nacho. Kiburi hicho ndicho kinachompeleka kwenye kifo kiovu baada ya kumuua babake na kumuoa mamake bila ya kujua. n nKatika tafsiri hii iliyofanywa kutokana na nakala kadha wa kadha za Kiingereza, Samuel Mushi ameuhifadhi ule moyo na tabia ya ushairi asilia wa Kigiriki na papo hapo akashikamana na mwendo wa ushairi wa Kiswahili kwa kadri inavyowezekana. Katika utangulizi wake anakokoteza kwamba ingawa mchezo huu ulitungwa kwa mujibu wa utamaduni wa Kigiriki wa kale, wahusika wake na hisia zao ni za kiulimwengu mzima na, kwa hivyo, mchezo wenyewe unaweza kuchezwa katika mazingira ya Kiafrika.

Kwenye Ukingo wa Thim

KShs375.00
Tamthilia ya Kwenye Ukingo wa Thim inaonyesha migogoro iliyopo baina ya mahitaji ya mila na mahitaji ya maisha ya kisasa. Mwandishi amefaulu kuonyesha mvutano huo unavyoweza kutokea na athari zake kwa wanaohusika.

Mashetani

KShs440.00
Kitaru na Juma ni vijana wawili ambao wanasoma katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, waniotoka katika familia mbili za kikabaila ambazo zenye historia zilizofanana na zilizotofautiana.Ukabaila wa familia ya Juma ni 'ubwanyenye', na ukabaila wa familia ya Kitaru ni 'unaizi'.Katika mchezo huu ukabaila wa aina ya familia ya Juma umeanza kung'olewa, lakini ukabaila wa aina ya familia ya Kitaru ndiyo kwanza unatiliwa mbolea na uzalendo. Daina ya Kitaru na Juma kuna mapenzi na chuki, shaka na wasiwasi, tuhuma na dhambi, huku wakitafuta uhusiano wa maana katika wakati na hali waliyonayo.

Msako Hatari

KShs500.00
Author: Halfani Sudy ISBN: “9780195747751”

Utashi wa Dola na Hadithi Nyingine

KShs590.00
Kila mtu hufanya juhudi ili apate kufaulu maishani. Katika hali hii, ahadi nyingi hutolewa, miadi ikapangwa na mikakati kuwekwa ili kufanikisha maazimio. 'Utashi wa Dola na hadithi nyingine' ni mkusanyo wa hadithi fupi zinazoakisi maisha ya wanadamu: hisia zao, mitazamo yao, ndoto zao, matumaini yao. Ubora wa hadithi katika mkusanyo huu haumo tu katika uanuwai wa fani bali pia kwenye mseto wa ufundi wa wachangiaji ambao wana asili na mitazamo tofauti. Aidha, hadithi hizi zimeteuliwa kwa upekee wa maudhui yanayoangaziwa, kama vile tamaa, nafasi ya mtoto wa kiume, ufisadi, dhuluma na unyanyasaji, ubinafsi, mapenzi, ndoa, usaliti miongoni mwa mengine mengi. n nHadithi hizi zimeandikwa na waandishi, mahiri na chipukizi, kutoka maeneo mbalimbali ya Afrika Mashariki. Mchango wao katika diwani hii ni wa kipekee na bila shaka utakupa kila sababu ya kuthamini uanuwai wa tamaduni zetu mbalimbali, zinazofanikisha umoja wetu.

Dunia Yao

KShs690.00
'Dunia Yao' ni riwaya inayothibitisha namna ujasiri wa mwandishi ulivyoimarika kwa kujadili mambo nyeti kuhusu jamii yake na mataifa. Tunakutana na Ndi- anayejifungia njozini kukimbia ukweli unaompa mateso na kuihangaisha akili yake. Mwishowe anaishiwa na kila kitu ila ishara za mauti. Kwa nini? Kitendawili hiki tunakuachia wewe msomaji ukitegue. n nUlimwengu wa riwaya hii na msuko wake, na umbo lake na muundo wake, kamwe si wa kawaida. Umetengenezwa kumvutia msomaji kwa njia ya ajabu. Ni wa majaribio yanayovunja sarufi au kanuni zote za lugha na sanaa ili ufanane na dunia tunayoishi leo. Dunia ambayo ni tata na ovyo, iliyobutuka, iliyoparaganyika, inayotuchezesha foliti za mauti, inayonata utamu wa kifo na uchungu wa uhai. Inamtafuta msomaji imnase mara anapokikamata kitabu.

Kanda ya Siri

KShs560.00
Chifu Abdullah anaingia katika kazi ngumu kuliko zote alizowahi kuzifanya katika maisha yake, kazi ya kuisaka kanda iliyopotea katika kasri yake. Kanda yenyewe inatembea kutoka mkono mmoja hadi mwingine, huku pande mbili zinazoisaka zikitumia nguvu, pesa na akili kuitafuta. n nMsako wa kanda unakutanisha watu wenye tajriba pana katika mambo ya uhalifu. Wapo wanaojeruhiwa, wapo wanaoumizwa, wapo wanaokufa kwa sababu ya kanda, hali inayoitia jeshi la polisi katika kibarua kigumu cha kuwasaka wahalifu hao. n nJe, polisi watafaulu kuwapata wahalifu hao. Je, kanda yenyewe itapatikana? Hivi, ndani ya kanda kuna nini?

Pigo la Nafsi

KShs475.00
"Halima mwanangu, wakati mwingine nashindwa kuelewa dunia inaelekea wapi. Visa kama hivyo ni vingi tu katika maisha yetu siku hizi. Ajabu ni kuwa, licha ya madhalimu hao kufikishwa mbele ya sheria, wao hufanya hila wakajipa uhuru." Matumaini ya familia ya Halima yanafufuka pale anapopata ajira kama mjakazi. Kwake Halima, anaiona fursa hii kuwa muhimu zaidi katika kutimiza maazimio yake na ndoto zake maishani. Maisha yanamwia mazuri Dar es Salaam hadi siku moja ambapo mambo yanaharibika na kumtia wasiwasi kuhusu mipango yake na mchumba wake. Je, ni mambo gani yaliharibika, na nani kayaharibu? n n'Pigo la Nafsi' ni hadithi inayosimuliwa kwa upekee wa namna yake. Hadithi hii imejaa mafunzo yanayoakisi uhalisia wa maisha, katika dunia ya sasa.

Mabandia

KShs375.00
'Mabandia' ni tamthilia inayopiga kurunzi ubandia unaojificha na kujifichua kwa sura mbalimbali maishani. Maisha ni kama karata. Wahusika sita wanajitokeza katika maonyesho sita wakifululiza hadi barazani kucheza duru sita za mchezo maarufu wa Wahedi wa Sitini. Mchezo huu huchezwa hasa katika maeneo ya pwani ya Afrika Mashariki. n nKupitia vitendawili vinavyoibuka katika maonyesho mbalimbali, mwandishi anagubika hoja kadhaa za ubandia. Hoja hizi zinalenga kutafakarisha jinsi ubandia huo unavyoathiri mitazamo ya binadamu katika nyanja mbalimbali za maisha. n nAli Attas ni mwandishi mtajika wa vitabu kadhaa vikiwemo kamusi, vitabu vya lugha na vilevile vya hadithi. Kama mhariri wa vitabu vya elimu, mtangazaji, mwandishi habari na mwalimu wa lugha na fasihi mwenye uzoefu mkubwa, amebugia tajriba pana na za kipekee katika ukumbi wa kukikuza Kiswahili.

Kamwe si Mbali

KShs550.00
"Tambo njoo unisaidie. Nimeshalishika lile jisamaki kubwa linaloogelea huru mawinguni bila ya kumeza ndoana limemeza ndoana ... Njoo unisaidie kulivuta jisamaki hili... Je, sikukwambia, Tambo, kwamba kamwe si mbali tena?" n nKatika riwaya hii kila kizazi kinapitia nyakati mbalimbali zinazoathiriwa na usasa. Ina hadithi za watu wanaolishana halua au shubiri. Ndani ya hadithi hizo mnaibuka usuria, utumwa, mapenzi motomoto, wakati wa mporomoko na wakati mpya, ukimbizi wa mtu-kwao, dini ya aina moja inayosimamia dini zote. Wanawake wanakusanya nguvu na hatimaye kukata minyororo. Zaidi ya yote hayo ni miujiza inayooneshwa na wahusika ... Haya yote yanasimuliwa na hadithi nyingi katika hadithi moja inayokuzwa na kurambishwa utamu wa lugha.

Tunu ya Ushairi

KShs525.00
'Tunu ya Ushairi' ni mkusanyo wa mashairi ya aina, maudhui na mitindo mbalimbali. Kuna mashairi arudhi, mashairi huru na mashairi picha. Diwani hii ina mashairi ambayo msomaji atajihusisha nayo kwa njia rahisi. Ujumbe wake unapitishwa kwa njia sahili na yenye mguso unaoiacha athari ya kudumu kwa msomaji. Washairi hawakujikita katika mikondo iliyopo tu; wamezuka na mikondo mipya ya utungaji wa mashairi arudhi ambayo itachangia kubadilisha mtazamo wetu kuhusu aina za mashairi. Mkusanyo huu unatoa changamoto kwa wahakiki wa fasihi kutathmini upya upya maelezo dhana mbalimbali za ushairi.

Beluwa

KShs390.00
Beluwa: ! Hukubisha? Unaingiaje hapa hivi hivi tu? Hujui kuwa huku kuna wenyewe? n nMiaka minne baada ya kukata rufaa, Beluwa bado yuko rumande. Anakutana ana kwa ana na ukweli baada ya kusombwa na wimbi kali la mkono wa sheria. Akiwa rumande anakutana na wafungwa wenzake; Tanda na Mtu. Ili kupitisha muda wakisubiri kusikilizwa kwa kesi zao, wanacheza michezo ya kitashtiti inayotalii kadhia zinazoumeza ulimwengu. 'Beluwa' ni mchezo wa kibwege unaoburudisha ajabu!

Othello

KShs490.00
Lago anaapa kulipiza kisasi kwa kuivuruga ndoa ya Othello na Desdemona. Njia pekee ya kufanikisha lengo lake ni kumghilibu Othello kuwa mkewe ni mwasherati. n nJe, Iago atafaulu katika azma yake? Je, Othello atazikubali hila za Iago? Endapo Othello atashawishika, atamchukulia hatua gani Desdemona? n nHaya ni kati ya maswali anayoyajibu William Shakespeare katika tamthiliya hii ya tanzia inayoburudisha, kufunza na kukaidi mpito wa wakati. Tafsiri hii imeandikwa kwa ufundi mkubwa hivi kwamba ule mvuto na mnato wa kazi asilia umedumishwa.