Showing 1–20 of 52 results

ABCh Herufi za Kiswahili by Nasra Oma...

KShs1,000.00 KShs780.00

A Swahili alphabet book suitable for native Swahili-speaking toddlers who are beginning to learn the alphabet and children of all ages who are learning Swahili.

Kitabu hiki kinawafahamisha watoto herufi na maneno ya Kiswahili. Kinawafaa watoto wachanga waliolelewa wakizungumza Kiswahili kujifunza herufi na watoto wa rika zote wanaoanza kujifunza Kiswahili.

Sinema ya Karate

KShs330.00
Kadiri anaingiwa na wasiwasi kutokana na mabadiliko katika tabia ya rafiki yake. Anashangaa anapomwona rafiki yake akitoweka kama moshi baada ya masomo ya kila siku kuisha. Kitendo cha rafiki yake kinamtia ari ya kutaka kufahamu ni kitu gani kinachomtoa mwenzake mbio. Juhudi zake za kutaka kujua anakoenda rafiki yake wakati wa mazoezi ya karate yanaambulia patupu. Kwa sababu hiyo, anaapa kufanya juu chini ili apate kujua kinachoendelea na sababu za rafiki yake kubadilika. n nJe, Kadiri atapata kujua kinachomfanya rafiki yake kubadilika? Je, atafanya nini ili kuweka wazi kinachoendelea? Je, ni nini kitatendeka atakapogundua kinachoendelea? nSinema ya Karate ni kisa cha kiupelelezi. Kisa hiki kinaangazia masuala ya malezi, elimu, uhifadhi wa mazingira miongoni mwa masuala mengine katika jamii. Kisa hiki kimesheheni mbinu na mitindo mbalimbali ambayo itamfaidi mwanafunzi katika kujenga lugha na ubunifu wake.

Sikukuu Nzuri

KShs205.00
Sikukuu Nzuri ni hadithi inayoangazia msamiati wa vyakula. Lola na wenzake wanajadili kuhusu chakula ambacho wangependa kula siku ya sikukuu. Je, watachagua vyakula gani? n nSoma Nasi ni msururu wa hadithi zilizoandikwa kwa kuzingatia mada mbalimbali. Hadithi hizi zitawawezesha wanafunzi wenye uwezo tofautitofauti kuimarisha stadi za lugha walizojifunza darasani. Wanafunzi watafurahia kuzisoma hadithi hizi kwa lengo la kujiburudisha na pia kufanya mazoezi ya stadi za lugha.

Temo dukani

KShs125.00
Vitabu katika Mradi wa Kusoma wa Simba vinalenga kuwapa wanafunzi wa chekechea msingi thabiti wa stadi ya kusoma. Vitabu hivi vinamlenga mwanafunzi ambaye anaanza kutambua herufi, silabi na maneno ambayo yanaweza kutambulika moja kwa moja. Vitabu hivi vina picha na urudiaji wa maneno ili kumsaidia mwanafunzi kusoma kwa wepesi. Kila hadithi ina wazo moja tu.

Mchoro wa Naseku

KShs100.00

Matunda ni Afya

Rama na Karembo

Michezo yetu

Masomo yetu

Pipi za Lona

Uhuru wa Jelani

KShs330.00
Je, unafikiri Jelani alihitaji uhuru wa aina gani? Je, ni nini kilichokuwa kimemsababishia ukosefu wa uhuru? Atafanya nini ili aweze kuupata uhuru huo? Je, atafanya nini iwapo ataupata uhuru huo? n nUhuru wa Jelani ni novela iliyosukwa kwa mtindo wa kipekee. Mwandishi ameyaweka bayana masuala ya kitamaduni ambayo yanaweza kutinga maendeleo ya mtoto msichana katika jamii ya leo. Novela hii imetumia mbinu anuai za lugha zinazoifanya hadithi yenyewe kuvutia na kumpa msomaji hamu ya kuendelea kusoma. Novela hii imeangazia masuala mtambuko mbalimbali na kusawiri maadili yanayopendekezwa katika Mtaala wa Daraja ya Awali ya Shule za Sekondari. n nKuhusu mwandishi n nWendo Nabea ni mtunzi wa tamthilia na bunilizi na kadhalika ni mhakiki wa fasihi. Ni mwelekezi, msahalishaji na mwamuzi katika Tamasha za Drama na Filamu na aidha Tamasha za Muziki za shule na vyuo nchini Kenya. Alipata shahada yake ya kwanza katika Chuo Kikuu cha Nairobi aliposoma Kiswahili na Fasihi ya Kiingereza na ambapo pia alisomea Uzamili. Baadaye alijiunga na Chuo Kikuu cha Vienna, Austria, kwa masomo ya Uzamifu. Hivi leo ni Profesa katika Chuo Kikuu cha Laikipia nchini Kenya anapofundisha Fasihi na Mawasiliano. Wendo Nabea ni mwandishi wa tamthilia Insha ya Siri iliyochapishwa na Shirika Ia Uchapishaji Ia Oxford.

Twala Wapi Leo?

KShs330.00
Tumalize anashangazwa na hatua ya baba yake kuwapa kitu fulani, watu fulani, kila siku asubuhi anapoenda shuleni. Kitendo cha baba yake kinamtia mshawasha wa kutaka kujua ni kitu gani hicho wanachopewa watu wale. Juhudi zake za kutafuta maelezo kutoka kwa baba yake kuhusu kitu hicho na sababu ya yeye kukitoa kwa watu wale zinagonga mwamba. Kwa sababu hiyo, anaapa kufanya juu chini ill apate kujua kitu hicho, na sababu inayofanya watu wale wapewe kitu hicho. n nJe, Tumalize atapata kujua kitu hicho wanachopewa watu hao? Je, atafanya nini ili kubaini kitu hicho? Je, ni nini kitatokea atakapopata kugundua kitu chenyewe? n nTwala Wapi Leo? ni kisa cha kusisimua cha kiupelelezi. Kisa hiki kinaangazia masuala ya malezi, elimu, ufisadi, ujasiriamali miongoni mwa masuala mengine katika jamii. Kisa hiki kimesheheni mbinu na mitindo mbalimbali ambayo itamfaidi mwanafunzi katika kujenga ubunifu wake na vilevile lugha yake. n nKuhusu mwandishi n nShullam Nzioka ni mwandishi, mfasiri, msawidi na ashiki wa lugha ya Kiswahili. Ameandika kazi mbalimbali za fasihi, zikiwamo novela, hadithi fupi na hadithi za watoto. Kitabu chake, Mbona Hivi? kilishinda tuzo ya Jomo Kenyatta Prize for Literature kitengo cha kijana mnamo mwaka wa 2021. Baadhi ya kazi zake zilizowahi kuchapishwa ni pamoja na Si Kitu na Shani ya Saa (hadithi fupi) iliyo katika kitabu Utashi wa Dola. Mbali na hayo, amewahi kufanya kazi katika shirika la International Bible Students Association.

Kiswahili Dadisi Mwongozo wa Mwalimu,...

KShs550.00
Mwongozo wa Mwalimu n nGredi ya 3 n nKiswahili Dadisi, Mazoezi ya Lugha ni msururu wa vitabu vilivyoandikwa kwa ustadi na upekee ili kutosheleza mahitaji ya Mtaala wa Umilisi. Vitabu katika msururu huu vitakusaidia kumwezesha mwanafunzi kupata umilisi wa lugha katika stadi za Kusikiliza, Kuzungumza, Kusoma na Kuandika kama ilivyopendekezwa katika Mtaala wa Umilisi. n nVitabu katika msururu huu vina mazoezi murua ambayo yatawachangamsha wanafunzi wako na kuwapa hamu ya kutaka kujifunza lugha. Mazoezi haya yanakuza umilisi uliopendekezwa, maadili na kufahamisha kuhusu masuala mtambuko. n nKiswahili Dadisi, Mazoezi ya Lugha, Mwongozo wa Mwalimu, Gredi ya 3 kina mifano halisi na ya kutosha kukuwezesha kuwasaidia wanafunzi kukuza umilisi unaokusudiwa. Katika mwongozo huu utapata: n
    n
  • utangulizi wa kina kuhusu Mtaala wa Umilisi
  • n
  • muhtasari wa umilisi, maadili, masuala mtambuko na shughuli nyinginezo zilizoratibiwa kufundishwa katika kila suala kuu
  • n
  • maelezo kuhusu jinsi ya kushirikisha vifaa vya kidijitali katika ufundishaji
  • n
  • mapendekezo ya majibu ya maswali yote katika Kitabu cha Mwanafunzi
  • n
  • mapendekezo ya shughuli za wanafunzi nje ya darasa
  • n
  • maelekezo ya kina kuhusu jinsi ya kutathmini wanafunzi.
  • n
nKiswahili Dadisi, Mazoezi ya Lugha, Kitabu cha Mwanafunzi, Gredi ya 3 pamoja na Mwongozo wa Mwalimu vina shughuli, mazoezi na maelekezo tosha ambayo yatakufaa sana ili kuwawezesha wanafunzi kufaulu katika Mtaala wa Umilisi. n nOxford, mshirika wako katika ufanisi!

Kiswahili Dadisi Mwongozo wa Mwalimu,...

KShs600.00
Mwongozo wa Mwalimu n nGredi ya 2 n nKiswahili Dadisi, Mazoezi ya Lugha ni msururu wa vitabu vilivyoandikwa kwa ustadi na upekee ili kutosheleza mahitaji ya Mtaala wa Umilisi. Vitabu katika msururu huu vitakusaidia kumwezesha mwanafunzi kupata umilisi wa lugha katika stadi za Kusikiliza, Kuzungumza, Kusoma na Kuandika kama ilivyopendekezwa katika Mtaala wa Umilisi. n nVitabu katika msururu huu vina mazoezi murua ambayo yatawachangamsha wanafunzi wako na kuwapa hamu ya kutaka kujifunza lugha. Mazoezi haya yanakuza umilisi uliopendekezwa, maadili na kufahamisha kuhusu masuala mtambuko. n nKiswahili Dadisi, Mazoezi ya Lugha, Mwongozo wa Mwalimu, Gredi ya 2 kina mifano halisi na ya kutosha kukuwezesha kuwasaidia wanafunzi kukuza umilisi unaokusudiwa. Katika mwongozo huu utapata: n
    n
  • utangulizi wa kina kuhusu Mtaala wa Umilisi
  • n
  • muhtasari wa umilisi, maadili, masuala mtambuko na shughuli nyinginezo zilizoratibiwa kufundishwa katika kila suala kuu
  • n
  • maelezo kuhusu jinsi ya kushirikisha vifaa vya kidijitali katika ufundishaji
  • n
  • mapendekezo ya majibu ya maswali yote katika Kitabu cha Mwanafunzi
  • n
  • mapendekezo ya shughuli za wanafunzi nje ya darasa
  • n
  • maelekezo ya kina kuhusu jinsi ya kutathmini wanafunzi.
  • n
nKiswahili Dadisi, Mazoezi ya Lugha, Kitabu cha Mwanafunzi, Gredi ya 2 pamoja na Mwongozo wa Mwalimu vina shughuli, mazoezi na maelekezo tosha ambayo yatakufaa sana ili kuwawezesha wanafunzi kufaulu katika Mtaala wa Umilisi. n nOxford, mshirika wako katika ufanisi!

Kiswahili Dadisi Mwongozo wa Mwalimu,...

KShs600.00
Mwongozo wa Mwalimu n nGredi ya 1 n nKiswahili Dadisi, Mazoezi ya Lugha ni msururu wa vitabu vilivyoandikwa kwa ustadi na upekee ili kutosheleza mahitaji ya Mtaala wa Umilisi. Vitabu katika msururu huu vitakusaidia kumwezesha mwanafunzi kupata umilisi wa lugha katika stadi za Kusikiliza, Kuzungumza, Kusoma na Kuandika kama ilivyopendekezwa katika Mtaala wa Umilisi. n nVitabu katika msururu huu vina mazoezi murua ambayo yatawachangamsha wanafunzi wako na kuwapa hamu ya kutaka kujifunza lugha. Mazoezi haya yanakuza umilisi uliopendekezwa, maadili na kufahamisha kuhusu masuala mtambuko. n nKiswahili Dadisi, Mazoezi ya Lugha, Mwongozo wa Mwalimu, Gredi ya 1 kina mifano halisi na ya kutosha kukuwezesha kuwasaidia wanafunzi kukuza umilisi unaokusudiwa. Katika mwongozo huu utapata: n
    n
  • utangulizi wa kina kuhusu Mtaala wa Umilisi
  • n
  • muhtasari wa umilisi, maadili, masuala mtambuko na shughuli nyinginezo zilizoratibiwa kufundishwa katika kila suala kuu
  • n
  • maelezo kuhusu jinsi ya kushirikisha vifaa vya kidijitali katika ufundishaji
  • n
  • mapendekezo ya majibu ya maswali yote katika Kitabu cha Mwanafunzi
  • n
  • mapendekezo ya shughuli za wanafunzi nje ya darasa
  • n
  • maelekezo ya kina kuhusu jinsi ya kutathmini wanafunzi.
  • n
nKiswahili Dadisi, Mazoezi ya Lugha, Kitabu cha Mwanafunzi, Gredi ya I pamoja na Mwongozo wa Mwalimu vina shughuli, mazoezi na maelekezo tosha ambayo yatakufaa sana ili kuwawezesha wanafunzi kufaulu katika Mtaala wa Umilisi. n nOxford, mshirika wako katika ufanisi!

Kiswahili Dadisi Kitabu cha Mwanafunz...

KShs600.00
Kitabu cha Mwanafunzi, Gredi ya 3 n nKiswahili Dadisi ni msururu wa vitabu vilivyoandikwa kwa utaalamu na upekee ili kutosheleza mahitaji ya mtalaa wa umilisi. Vitabu hivi vitamwezesha mwanafunzi kupata ufahamu wa lugha kupitia stadi za Kusikiliza na Kuzungumza, Kusoma na Kuandika, na vilevile Sarufi. Aidha, vina mazoezi murua ambayo yatampa mwanafunzi hamu ya kujifunza. Pia, vinakuza umilisi utiopendekezwa, maadili na kufahamisha kuhusu masuala ibuka. Katika Kiswahili Dadisi, Kitabu cha Mwanafunzi, Gredi ya 3, utapata: n
    n
  • mada zilizopangwa kwa kuzingatia muainisho wa mtaala mpya.
  • n
  • mifano halisi ya miktadha ambapo lugha hutumika.
  • n
  • mazoezi ya kuwahamasisha wanafunzi kuendeleza ujifunzaji nje ya darasa na yale yenye kuwashirikisha katika shughuli za kijamii zinazokuza ujifunzaji.
  • n
  • mazoezi yanayomhusisha mwanafunzi moja kwa moja.
  • n
  • mazoezi yanayompa mwanafunzi fursa ya kujitathmini.
  • n
nKiswahili Dadisi, Kitabu cha Mwanafunzi, Gredi ya 3 kina Mwongozo wa Mwalimu ambao pia una mazoezi na maelekezo tosha ambayo mwalimu atahitaji ili kumwongoza mwanafunzi aweze kufaulu katika mtalaa huu mpya wa umilisi.

Kiswahili Dadisi Kitabu cha Mwanafunz...

KShs600.00
Kitabu cha Mwanafunzi, Gredi ya 2 n nKiswahili Dadisi ni msururu wa vitabu vitivyoandikwa kwa utaalamu na upekee ili kutosheleza mahitaji ya mtataa wa umilisi. Vitabu hivi vitamwezesha mwanafunzi kupata ufahamu wa lugha kupitia stadi za Kusikiliza na Kuzungumza, Kusoma na Kuandika, na vilevite Sarufi. Aidha, vina mazoezi murua ambayo yatampa mwanafunzi hamu ya kujifunza. Pia, vinakuza umilisi utiopendekezwa, maadili na kufahamisha kuhusu masuala ibuka. n nKatika Kiswahili Dadisi, Kitabu cha Mwanafunzi, Gredi ya 2, utapata: n
    n
  • mada zilizopangwa kwa kuzingatia muainisho wa mtaala mpya.
  • n
  • mifano halisi ya miktadha ambapo lugha hutumika.
  • n
  • mazoezi ya kuwahamasisha wanafunzi kuendeleza ujifunzaji nje ya darasa na yale yenye kuwashirikisha katika shughuti za kijamii zinazokuza ujifunzaji.
  • n
  • mazoezi yanayomhusisha mwanafunzi moja kwa moja.
  • n
  • mazoezi yanayompa mwanafunzi fursa ya kujitathmini.
  • n
nKiswahili Dadisi, Kitabu cha Mwanafunzi, Gredi ya 2 kina Mwongozo wa Mwatimu ambao pia una mazoezi na maelekezo tosha ambayo mwalimu atahitaji ili kumwongoza mwanafunzi aweze kufaulu katika mtalaa huu mpya wa umilisi.

Kiswahili Dadisi Kitabu cha Mwanafunz...

KShs580.00
Kitabu cha Mwanafunzi, Gredi ya I n nKiswahili Dadisi ni msururu wa vitabu vitivyoandikwa kwa utaatamu na upekee ili kutosheleza mahitaji ya mtataa wa umilisi. Vitabu hivi vitamwezesha mwanafunzi kupata ufahamu wa lugha kupitia stadi za Kusikiliza na Kuzungumza, Kusoma na Kuandika, na vilevite Sarufi. Aidha, vino mazoezi murua ambayo yatampa mwanafunzi hamu ya kujifunza. Pia, vinakuza umilisi utiopendekezwa, maadili na kufahamisha kuhusu masuala ibuka. n nKatika Kiswahili Dadisi, Kitabu cha Mwanafunzi, Gredi ya I , utapata: n
    n
  • mada zilizopangwa kwa kuzingatia muainisho wa mtaala mpya.
  • n
  • mifano halisi ya miktadha ambayo lugha hutumika.
  • n
  • mazoezi ya kuwahamasisha wanafunzi kuendeleza ujifunzaji nje ya darasa na yale yenye kuwashirikisha katika shughuti za kijamii zinazokuza ujifunzaji.
  • n
  • mazoezi yanayomhusisha mwanafunzi moja kwa moja.
  • n
  • mazoezi yanayompa mwanafunzi fursa ya kujitathmini.
  • n
nKiswahili Dadisi, Kitabu cha Mwanafunzi, Gredi ya I king Mwongozo wa Mwatimu ambao pia una mazoezi na maelekezo tosha ambayo mwatimu atahitaji ili kumwongoza mwanafunzi aweze kufaulu katika mtataa huu mpya wa umilisi. n nOxford, mshirika wako katika ufanisi!

Kivuli Kinaishi

KShs460.00
'Kivuli Kinaishi' ni tamthilia iliyoandikwa kwa kutumia dhana ya Giningi; makazi yaliyo ndani ya vichwa vya watu wa Unguja na Pemba na ambayo yanaogopwa sana na kuhusishwa na vitisho na hadithi kadhaa. Serikali ya Giningi yenye amri moja tu inaongozwa na Bi. Kirembwe akisaidiwa na wazee. Amali kuu ya Giningi imeonyeshwa kuwa ni ukatili na hivyo kanuni kubwa ni kujaribu kuwatoa watu kutoka dunia hii tuijuayo na kuwapeleka katika dunia ya siri, Giningi. Mwandishi amefaulu sana kutumia U-giningi katika kuchora picha fulani tata inayofanana na Giningi. Mhusika Mtolewa anadhihirisha mapambano ya kifikra yanayotokea kati ya wana-Giningi na Bi. Kirembwe na kuonyesha bayana mchezo huu unavyoambatana na ukweli wa maisha, na zaidi jinsi ulivyo mchezo wa wakati.

Sauti ya Dhiki (Toleo Jipya)

KShs440.00
Diwani hii - inayosheheni mashairi kuhusu utamaduni, mapenzi, nasaha, siasa, mambo ya kinyumbani, n.k. - ilitungwa baina ya 1969 na 1972 ambapo mtunzi alikuwa kifungoni baada ya kupatikana na hatia ya kuwachochea watu ili waipindue Serikali ya Kenya kwa kutumia silaha. Kwa hivyo, unapoisoma diwani hii hutaweza kujizuia kuona athari ambayo kifungo huweza kuwa nayo kwa mfungwa. n nJambo la maana sana kuhusu diwani hii ni kwamba mtunzi ameweza kuzungumzia mambo ya kisasa, kama alivyofanya katika shairi la 'Usiniuwe!', bila kupotoka na kutafuta mifano ya kigeni. Hili ndilo lililompa Shihabuddin Chiraghdin, mmoja wa wataalamu mashuhuri wa lugha ya Kiswahili, kusema katika utangulizi wake kwamba, ingawa mtunzi ameingiliwa na athari za kigeni kwa ajili ya elimu aliyoipata shuleni, 'hakukubali kuzongwazongwa na athari hizo, hivyo mashairi yake hayana maingilio ya miundo ya kigeni hata chembe, na mawazo yake yote yameambatana na Uswahili na Uafrika kwa jumla'. n nKitabu hiki kitawafaa wale wapendao kusoma mashairi ya Kiswahili ya kiwango cha juu, na vilevile wanafunzi wa fasihi ya Kiswahili katika shule za sekondari na vyuo vikuu.